July 15, 2020


PAUL Godfrey, beki wa kulia leo ameifungia timu yake bao la kwanza ndani ya msimu wa 2019/20 ndani ya Ligi Kuu Bara wakati wakishinda mabao 3-1 mbele ya Singida United.

Mchezo huo wa ligi ulichezwa leo Julai 15 Uwanja wa Taifa na kuwafanya Yanga wasepe na pointi tatu.

Bao la pili lilipachikwa na Mrisho Ngassa alipachika bao la pili dakika ya 37 akimalizia pasi kutoka kwa Deus Kaseke.

Mwili jumba dakika ya 68 Ikpe Gnamien alipachika bao la tatu baada ya kumpiga chenga kipa wa Singida United na kuwafanya Yanga waifunge jumla ya mabao 3-1 Singida United.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Liti, Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 ambayo yamejirudia tena Uwanja wa Taifa. 

Ushindi huo unaifanya Yanga kujikita nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 baada ya Azam FC kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa bao 1-0.

Azam FC inashushwa mpaka nafasi ya tatu ikiwa na pointi zake 67 kibindoni.

Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 35 ambapo bao la kufutia machozi lilifungwa na Stephen Sey 45.

2 COMMENTS:

  1. Nilitarajia timu yangu itaitwanga Singida timu ambayo imeshateremka daraja itaitwanga kama ble walivoitwanga Simba na Azam kwa magoli yasiyohezabika lakini badala yake tukaishuhudia Singida kumiliki mpira vyema na kuliandama lango letu. Inatuumiza sana

    ReplyDelete
  2. Wefyatu kweli ko singida walikua wamekaa tu hawachezi nahsi hujui nn maana ya mpira

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic