August 8, 2020

BERNARD Morrisom kiungo mshambuliaji ambaye leo ametambulishwa ndani ya Simba kwa dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Yanga amesema kuwa hakuna haja ya mashabiki kumlaumu kwa kuwa ni sehemu ya kazi yake.


Morrison alikuwa kwenye mvutano mkubwa na Yanga kwenye ishu ya mkataba ambapo yeye alikuwa anasema kuwa anamkataba wa miezi sita ambao umekwisha huku uongozi wa Yanga ukieleza kuwa bado nyota huyo alikuwa anadili la miaka miwili.


Baada ya Simba kumtangaza Morrison, Yanga nao walitoa tamko kuwa wanafuatilia suala hilo ili kujua ukweli ili wachukue hatua kuhusu suala hilo kwa kuwa bado ana mkataba mpaka 2022.


Akizungumza muda mfupi kabla ya mchezo wa hisani unaochezwa muda huu, Uwanja wa Mkapa kati ya TimuKiba na TimuSamatta huku yeye akiwa ni mchezaji wa TimuSamatta, Morrison amesema:"Najua wengi wanasema kuhusu mimi mashabiki wanakasirika lakini hakuna baya, huu ni mpira na hii ni kazi yangu.

"Naiheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na ina uwezo mkubwa nami pia ninajua kwamba Simba ni timu kubwa na ina mashabiki wake hivyo ni mwendelezo wa kazi," amesema. 


Chanzo:Azam TV  

23 COMMENTS:

  1. Uyo mpuuzi atokaa acheze mpira kwa amani apa Tanzania labda aijui vizuri yanga,akuna mchezaji aliyewai kuondoka yanga kwa dharau na nyodo kama uyu na akafanikiwa uko aendako, xaxa tff na simba wameshirikiana ktk hili ndo maana tiyali wamewaambia simba hukumu ilivyo wakamsainisha kabla ya hukumu kutoka hiyo ni dharau ya hali ya juu,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hukumu haitatoka maana hakuna kesi ya kujibu

      Delete
    2. Yanga ndio nani mpaka asicheze mipra kwa amani we ndimu kweli kawatishe wendaazimu wenzako

      Delete
  2. Waambie viongozi wako wakuonesha aliposaini hiyo miaka miwili.

    Mmechagua viongozi wasanii, tegemeeni timu na utendaji wa usanii.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lkn kweli kuondoa utata inabidi huo mkataba aliosaini miaka miwili uwekwe hadharani.Hivi kweli viongozi wa Simba watakuwa mazuzu kumsanisha Morissoni bila kujiridhisha huko kote kunakohusika? Msiwatupie lawama viongozi wa Simba bila kuangalia upande wa pili wa shillingi ndio utoe hukumu.Nahisi ni Yanga wenyewe wanasalitiana na kikulacho kinguoni mwako.

      Delete
  3. Viongozi wa Yanga acheni usanii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnabadilisha appearance ya picha mimi shahidi nimewakamata futeni

      Delete
    2. Pole braza naona unaota ndoto za alinacha. ni yeye ni yeye

      Delete
  4. kitendo Cha Simba kufanya usajili kwa Morrison na wanajua Kuna mgogoro na TFF haijatoa tamko ni dharau na ni njama za kuihujumu yanga.hapa ndo tuone TFF nguvu yake iko wapi au wote ni walewale?

    ReplyDelete
  5. mwana kulitafuta ....Yanga walianza huu mchezo kwa kujifanya wanamsajili Chama kwa maneno.sasa wameonyeshwa namna vitendo vinafanywa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnajaribu kulipa kisasi cha Mbuyu Twite japo baaaaaado sana hamjafika.Kwa namna hiyohiyo mlivyomlivyomchukua huyo ndivyo namna hiyohiyo atakavyowaacheni.Tunawashukuruni saaaaana kwa kutuondolea huyo mjinga,Yanga aliikuta na ameiacha.Kazi kwenu kumfuga mbwa asiyefugika.

      Delete
    2. 😆😆😆😆 maneno ya sitaki mbichi hizo hayo, viongozi wasanii mpaka wanachama,madhabiki na wanazil wote wasanii, mtalia mtoe machozi ya damu na bdo ndo mtaisikia refioni vidume wakiendelea kutusua bongo na kimataifa

      Delete
    3. Kwa hiyo unakubali kuwa Morissoni hakuwa na mkataba na Yanga wa miaka miwili kama mwenyewe alivyokuwa anasisitiza.Je Simba alienda kushitaki TFF kuwa Morissoni hana mkataba wa miaka miwili? Simba ana kosa gani kama ameshapata uhakika kuwa Morissoni hajasaini mkataba wa miaka miwili Yanga? Kwa nini Simba isimsainishe fasta kwani dirisha la usajili liko wazi tokea 1st hadi 31st Aug.Tatizo liko kwa viongozi wa Yanga bado hawajakomaa na fitina za soka la Tanzania.Warudi kuwauliza kina Seif Magari,Mkemi,Dr.Chanji, Jerry Muro nk ndio saizi ya kina Hans Pope,kaburu

      Delete
  6. Ya yanga tuwaachie wenyewe,kama hayakuhusu uondoke humu, iko siku yenu pia.

    ReplyDelete
  7. Simba haitokaa ifanikiwe kimataifa, unajua kwann?
    Wamezoea humu ndani kuhonga honga OFF, marefa, na kadharika.Ila niwambie tu ukweli kwamba kwa hapa ndani mtaendelea kuchikua ubingwa kwa kununua mechi na kuhonga lakini kwa nje ni mwendo wa khamsa makuma nyie.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama mlivyohonga marefarii mkapigwa 4G.

      Delete
    2. Kwani mnaojiita mabingwa wa kihistoria mmeshachukuwa makombe mangapi ya nje, maana mnajifanya watakatifu! Acheni ubabaishaji mpira hauendeshwi kwa bakuli dunia ya sasa.

      Delete
    3. Hata yanga tuwanunua na kuwapiga 4g

      Delete
    4. Ata Al Ahly si walikuwa wanaonga marefa ndio mana wakafungwa 6-0 NA Mamelodi Sundown hata wale waliofungwa 8-1 na Tp Mazembe nao huwa wanaonga marefa kwao kule Tunisia nyinyi ambao amuongi marefa mshawahi kufika hatua gani ligi ya mabingwa ndo mana mnaitwa Manyani f.c kwa kuwa akili zenu zinafanania na hao

      Delete
    5. Ila Yanga ndo itafanikiwa kimataifa kwa kuwa yenyewe huwa inafungwa 6-0 na Raja Casablanca, 4-0 Manning Rangers ya south Africa 5-0 dhidi ya simba ya Tanzania eti mwendo wa khamsa khamsa aya uyo aliyetufunga sisi hamsa yeye alifika wapi ndio mana mtu akikwambia akili zako kama mshabiki wa Yanga pigana

      Delete
  8. Kama ni kweli Morrison amepitishwa kimagumashi kwenda Simba kwasababu tu Waziri Mkuu, TFF, Bodi ya Ligi ni wanachama na Mashabiki wa Simba wamepindisha kanuni ili aende Simba. Wanayanga wamejiapiza "HAWATAMPIGIA KURA JPM KWENYE UCHAGUZI MKUU!

    ReplyDelete
    Replies
    1. JPM hataki hata kura yenu moja chizi we na tunashinda uchaguzi umweu wako peleka uko uko

      Delete
  9. hahahaaa! bonge la filamu naikumbuka na ile ya okwi! hataree

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic