August 9, 2020

 

MUDA mfupi baada ya aliyekuwa  Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba , Senzo Mbatha leo Agosti 9 kutangaza kujiuzulu nafasi yake katika klabu hiyo, huku akiishushukuru klabu kwa mafanikio yaliyopatikana kwenye kipindi kifupi inaelezwa kuwa amepewa kazi ndani ya Yanga.

Ofisa Uhamasihaji wa Yanga, Antonio Nugaz alitupia tweet ya Senzo ambayo ilikuwa inaeleza kuwa amejiuzulu nafasi yake ndani ya Simba huku akiisindikiza na maneno kuwa anaimani atamuona hivi karibuni jambo lililozua mjadala.

Senzo ameonekana akiwa na wadau wa Yanga jambo ambalo limetoa tafsiri kwamba amepewa kazi ndani ya timu hiyo ya watani wa jadi.

Alipotafutwa Senzo ili aweze kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo simu yake ilikuwa haipatikani huku viongozi wa Yanga wakigoma kutolea ufafanuzi jambo hilo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ukurugenzi Simba, Mohamed Dewji amesema kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram:"Tumetoka mbali na bado safari inaendelea, tumepita mengi Wana Simbawenzangu. 

"Nawaomba WanaSimba wote mtulie. Simba ni kubwa kuliko mtu mmoja. Sisi viongozi tunawatumikia usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bali Simba. Kazi inaendelea tuko imara,"



21 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Ukiangalia kwa makini basi utajua viongozi wa Yanga wamechamka kwa Morrisoni na hii ni kama kweli yanga wameingia makubaliano ya kimkataba na aliekuwa CEO wa Simba. Kwanini viongozi wa Yanga na wafadhili wao watumie Nguvu kubwa kupita kiasi yaani unaweza kusema wanatumia nguvu kubwa kunyume na uwezo wao kufanya propaganda za kuingia mktaba na Senzo ili iwe nini? Jibu rahisi hapa ni kwa viongozi wa Yanga kuwatuliza mashabiki wao wenye hasira baada ya kudanganywa na kumpoteza Morrisoni. Unaona kabisa viongozi wa Yanga wapo kwenye mcheheto wa hali ya juu kuhusiana na suala la Morrisoni.Mara sijui Deo kanda mara sijui mchezaji huyu. Kwa kweli kuna harufu mbaya inayoashiria ubabaishaji wa uongozi ndani ya klabu ya Yanga.

      Delete
    2. POle sana!!! Na bado!!!

      Delete
  2. Wale upande wa pili, laana zimeanza?

    ReplyDelete
  3. Yaani hii ndio ilikuwa ya kusimamisha nchi, au kuna nyingine?

    ReplyDelete
  4. Wale wa upande wa pili laana zimeanza?

    ReplyDelete
  5. Yeye ndo atalishugulikia suala la Morrison na anajua uchafu wote na waliohusika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Suala la Morrison lilishashughulikiwa TFF, watu walishachungulia majibu ya vipimo, endelea kusubiri

      Delete
  6. Laana labda kajilani mwenyewe? Yeye ni mwajiriwa kama maafisa wengine tu wa Simba, Na watu kama yeye wako wengi sana. Yeye alikuwa ni mtendaji tu, wenye maamuzi na dira ya clabu ni Simba@Modewji team.

    ReplyDelete
  7. Angalienitu siku mkipigwa 4G nyingine msije mkamrushia chupa za mikojo, Msije mkasema kauza mechi.

    ReplyDelete
  8. Hongereni msio jitambua wala kusoma alama za nyakati endeleeni kushabikia ujinga napesa za mo bila hata kutafakari mambo

    ReplyDelete
  9. Huyu alitaka alete wachezaji kama wale wa Brazil watatu ambaye mmoja tu alikuwa mchezaji wengine alikula.Aliposhtukiwa kwenye mambo ya usajili kelele zikaanza.Morrison hskywa na uamuzi vsli bofi ilitoa uamuzi. Akaona nongwa .Ni mwajiriwa aliyepita timu nyingi.

    ReplyDelete
  10. Huo ni mkataba au makubaliano, Maana siku hizi kuna watu wa mikataba na wazee wa makubaliano. Mwanzo utasiki ni mkataba mambo yakiharibika utasikia yalikuwa ni makubaliano.

    ReplyDelete
  11. Hivi kibali cha Senzo cha kufanya kazi Tanzania kilikuwa ni cha muda gani? Na je kiliainisha mwajiri ambaye angekuja kufanya kazi naye?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata mimi najiuliza kuna sheria za nchi huwezi kupewa kibali cha kazi halafu ukabadili kazi wakati kibali chako kinasema vingine

      Delete
  12. CEO tu mmechanganyikiwa je tungemchukua mchezaji wenu si mngejinyeaaa ovyo ovyoooo . mnateseka na CEO kweli nyie BATA kweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnaoteseka nyinyi mnaosema Morrison hatakaa acheze mipra kwa mani Tz hii we ushasikia mshabiki wa simba akimlilia Cenzo ila siwalaumu kwa sababu akili zenu si kama za Kima kwa ndo hivyo inabidi tuishi na nyinyi kama ndugu tutafanyaje sasa ndugu yako akiwa chizi utamkataa

      Delete
  13. mnateseka na CEO kweli nyie BATA kweli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic