TAYARI mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, na Kombe la FA wamemalizana na nyota wanne wa kazi ambao msimu ujao watakuwa na uzi mwekundu.
Baada ya dirisha la usajili kufunguliwa, Agosti Mosi, tayari Simba nao wameingia sokoni kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21.
Nyota wake wanne ambao wameshasaini dili la miaka miwili ni pamoja na Ibrahim Ame ‘Varane’ akitokea Coastal Union ya mkoani Tanga, Charles Ilanfya akitokea KMC, David Kameta,'Duchu' na Bernard Morrison akitokea Yanga.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wataendelea kufyatua vitu ndani ya mwezi huu wa usajili mpaka pale watakapoona inatosha.
"Mwezi Agosti wakati wa dirisha la usajili tutafyatuafyatua vitu na kuumiza roho za watu hivyo wasijali tupo vizuri sisi ni mabingwa na mimi ni msemaji wa timu kubwa lazima niongee kwa umakini," amesema.
Sawa De la Boss
ReplyDeleteKama ni kweli Morrison amepitishwa kimagumashi kwenda Simba kwasababu tu Waziri Mkuu, TFF, Bodi ya Ligi ni wanachama na Mashabiki wa Simba wamepindisha kanuni ili aende Simba. Wanayanga wamejiapiza "HAWATAMPIGIA KURA JPM KWENYE UCHAGUZI MKUU!
ReplyDeleteTanzania inakaribia watu milioni 57, simba tumeshafika milioni 38 na ushee. Hata yanga wote mkimsusia JPM kura za wanasimba zinatosha na pale mnapotarajia kuanza ujenzi wa uwanja panakwenda kujengwa sheli ya wilaya
DeleteHuwezi unganisha siasa na mpira dogo, muda mwingine huwa unaandika vitu vyenye maana na mantiki alakin kwa ujumbe huu umevuka mipaka jitahidi kuwa makini mdogo wangu hapa twazungumzia mpira sio siasa wala viongozi wa siasa.
ReplyDeleteKwani unafikiri aliyewaita uneducated alikosea
Deletekwani shida iko wapi?......nawashauri yanga wafanye usajiri wenye tija sio upuuzi wa kina Morrison
ReplyDeleteHuyu Alec anajulikana. Muda wote ni uchochezi lakini sasa ameanza kuvuka mipaka. Hilo la kususia ongelea mwenyewe wacha kuwaingiza wasiohusika. Ikibainika hakuna mkataba wa kisheria baina ya Morrison na Yanga utaweka wapi uso wako?Wacha kukurupuka kama ngiri aliyekurupushwa.
ReplyDeleteYanga mnakopa wachezaji.mtakula jeuri yenu
ReplyDelete