RASMI Kampuni ya GSM chini ya Mkurugenzi wa Uwekezaji, Injinia Hersi Said imesema kuwa wachezaji wao wa kimataifa wataanza kutua Agosti 15, mwaka huu mara baada ya anga za nchi mbalimbali kufunguliwa.
Wachezaji wa kimataifa wanaotajwa kujiunga na Yanga ni Wakongomani, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe wote wanaoichezea AS Vita ya DR Kongo, Michael Sarpong (huru), Erick Rutanga aliyekuwa anakipiga Rayon Sports na Jesse Were wa Zesco United.
Yanga tayari imeanza michakato ya usajili ambayo tayari imefanikisha usajili wa mabeki Bakari Mwamnyeto, Yassin Mustapha,Abdalah Shaibu,'Ninja' , kiungo Zawadi Mauya na mshambuliaji Waziri Junior.
Kwa mujibu wa Hersi zaidi ya asilimia 60 wameshamalizana na wachezaji kutoka nje ya na wanachosubiria ni kufunguliwa kwa anga zao nchi zao ambazo wachezaji wanatokea huko.
Hersi alisema wamefanya mawasiliano na nchi hizo na kupata taarifa anga zao zitaanza kufunguliwa Agosti 15, mwaka huu ndiyo siku hiyo vifaa vyao vipya vitanza kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wa jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa hivi sasa wanaendelea na usajili wa wachezaji wazawa baada ya kukamilisha wachezaji watano, lengo ni kusuka kikosi imara kitakacholeta ushindani mkubwa wa namba.
“Agosti 15, mwaka huu ndiyo anga zitaanza kufunguliwa kutokana na janga la Corona kwenye nchi ambazo wachezaji wetu tuliokuwa nao kwenye mipango ya kuwasajili katika kuelekea msimu ujao.
“Hiyo ni baada ya kufikia muafaka mzuri wa kufanya mazungumzo na kukubaliana," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment