August 2, 2020



LEO Agosti 2, Uwanja Nelson Mandela tutashuhudia
fainali ya kibabe ya Kombe la Shirikisho kati ya
Simba dhidi ya Namungo ambao unasubiriwa kwa shauku
kubwa na mashabiki.

Mshindi wa mchezo huu anapata nafasi ya
kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la
Shirikisho Afrika kwa kuwa Simba wao ni mabingwa
wa Ligi Kuu Bara na wana nafasi ya kushiriki Ligi ya
Mabingwa Afrika basi ikitokea wakashinda nafasi ya
kimataifa itawakilishwa na Namungo.

Ila mpaka sasa wakati wakiwa hawajacheza mchezo huo tayari tiketi ipo kwa Namungo hivyo ina uhakika wa kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Ikiwa taji litabebwa na Namungo, Simba itaishia
kubeba medali na kuskilizia tena kujipanga wakati
ujao endapo wataweza kutinga hatua ya fainali.

Hapa tunakuletea namna hesabu za timu hizi mbili ambazo zinakutana leo zilivyokuwa tangu awali mpaka kufikia leo kwenye fainali:-

Safari ya Simba ilikuwa namna hii:-Mzunguko wa 64,
Simba SC 6-0 Arusha United, Desemba 21, Uwanja wa Uhuru. Mzunguko wa 32, Simba 2-1 Mwadui,
Uwanja wa Uhuru.Hatua ya 16 bora, Stand United 1-
1 Simba,ilishinda kwa penalti 3-2 Uwanja wa
Kambarage, Shinyanga.Robo fainali , Simba 2-0
Azam FC, Uwanja wa Taifa, Julai Mosi.Nusu fainali,
Simba 4-1 Julai 12, Uwanja wa Taifa.

Namungo mwendo wao ulikuwa hivi:- Mzunguko wa
64, Namungo FC 1-0 Green Warriors, Desemba 22,
Uwanja wa Majaliwa. Mzunguko wa 32 bora,
Namungo FC 2-1 Biashara United, Januari
26,Uwanja wa Majaliwa.Mzunguko wa 16 bora,
Mbeya City 1-2 Namungo FC, Februari 25, Sokoine,
Mbeya. Robo fainali, Namungo 2-0 Alliance FC,
Uwanja wa Majaliwa, Juni 30. Nusu fainali, Julai 11,
Sahare All Stars 0-1 Namungo Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga.


Ubora wa Simba

Simba imekuwa imara kwa upande wa safu ya
ushambuliaji ambapo kwenye mechi zake tano
ambazo ni sawa na dakika 450 imefunga mabao 15
ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya
dakika 30.Ikiipoteza ile ya Namungo ambayo

imefunga mabao nane ikiwa na wastani wa kufunga
bao moja kila baada ya dakika 56.

Ubora wa Namungo upo kwenye safu ya ulinzi
ambapo imefungwa mabao mawili ikiwa na wastani
wa kuokota nyavuni mpira kila baada ya dakika 225
huku Simba ikifungwa mabao matatu ikiwa na
wastani wa kuokota mpira nyavuni kila baada ya
dakika 150.

Watakaokosekana

Kwa upande wa Simba wachezaji ambao
wanatarajiwa kukosekana ni wale ambao hawakuwa
kwenye mechi mbili za mwisho kati ya Simba v
Coastal Union na Simba v Polisi Tanzania kwa kuwa
hawapo kwenye mpango wa kocha. Ila wengine
wote walio na kikosi wapo fiti.

Wachezaji wao wanatakaoikosa fainali ni
Ibrahim Ajibu, Rashid Juma, Tairone Santos,Sharaf
Shiboub, Haruna Shamte hawa walikosekana
kwenye mechi mbili zilizopita kwa kuwa waliachwa
Dar es Salaam na mpaka sasa wapo Dar watawashuhudia kwa tv.

Kwa upande wa Namungo FC, Relliats Lusajo,
George Makanga na Steve Nzigamasabo hawa
wataukosa mchezo kwa kuwa wanaumwa na hawana mechi fitness huku Edward
Manyama,Stephen Duwa na Hashim Manyanya
kuanza kwao kikosi cha kwanza itategemea
maendeleo za hali zao kiafya.

Silaha za kazi

Timu zote mbili zinategemea viungo kwenye
kuamua matokeo na kuchezesha timu kutokana na
mbinu ambazo zinatumika kwa makocha hao.
Simba silaha namba moja na Clatous Chama kwa
upande wa viungo ambapo yeye ni kinara wa
kutengeneza mipango ndani ya Simba kwenye
kombe la Shirikisho na ni namba moja kwa kucheka
na nyavu.

Ana pasi tatu za mabao na amefunga
mabao manne ndani ya Kombe la Shirikisho.
Lukas Kikoti ni kiungo machachari ndani ya
Namungo ambaye amekuwa akimpa hofu kubwa
Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck
kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja.
Kwenye Ligi Kuu Bara ametengeneza jumla ya pasi
saba na kufunga mabao manne na Sven anajua
shughuli yake.

Waskie makocha

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba
amesema kuwa wanahitaji
ushindi ili watimize malengo yao.
“Utakuwa ni mchezo mgumu ndio maana ikaitwa
fainali ila tupo tayari kupata matokeo chanya ili
tutimize malengo yetu.”

Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo
amesema :”Ni ngumu
kucheza na mabingwa ambao wachezaji wake wote
wapo vizuri lakini haitupi mashaka nasi tupo vizuri
tunahitaji ushindi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic