Mabosi hao wameafikiana kwa pamoja kuwa wamalizane fasta na Ambundo ambaye amemalizana na Gor Mahia baada ya msimu huu kumalizika ambapo klabu hiyo imemruhusu kutua sehemu yoyote kutokana na mkataba wake kuisha.
Yanga wanamuangalia straika huyo kama mbadala wa David Molinga ambaye inatajwa kumalizana na RS Bercane ya Morocco.
Habari ambazo Spoti Xtra limezipata ni kuwa, Yanga wapo mstari wa mbele kumalizana na staa huyo wa zamani wa Alliance ya Mwanza.
“Kwa sasa hesabu ni kuona Ambundo anakuwa miongoni mwa wachezaji ambao watavaa uzi wa Yanga kwa msimu ujao ambapo mipango hiyo inaendelea taratibu.
“Imekuwa rahisi kumpata kwa sababu tayari ameshamalizana na Gor Mahia ambapo alikuwa akicheza baada ya mkataba wake kumalizika, hivyo kwa sasa yupo huru.
“Tunachotaka kuona ni kwamba kabla ya wiki mbili zile za mapumziko kumalizika basi kila kitu kiwe kimekamilika na aungane na wenzake mapema kwa ajili ya kambi kwa sababu yupo hapa nchini,” kilisema chanzo.
Hivi karibuni, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa wameshamaliza usajili wao kwa asilimi 90 kwa kufuata ripoti waliyoachiwa na aliyekuwa kocha wao, Mbelgiji Luc Eymael.
Goal wasingemuacha vijana wa kutengeneza timu ubingwa bado sana
ReplyDeleteGormahia
ReplyDeleteKaribu kijana upige kazi uwanja ni wako
ReplyDeleteHawa ni waongo wanatunga tu habari
ReplyDeleteYanga tengenezeni timu acheni kuangalia mchezaji alieko huru
ReplyDelete