MYKONOS, Ugiriki
NAHODHA wa Manchester United, Harry Maguire, anatuhumiwa kutoa rushwa kwa polisi baada ya kukamatwa nchini Ugiriki ambapo atapelekwa kwenye Kisiwa cha Syros kujibu tuhuma hizo akitokea Mykonos sehemu tukio lilipotendeka.
Staa huyo ambaye analipwa pauni 190,000 kwa wiki, baada ya kukamatwa alilala ndani pamoja na wenzake wawili baada ya kuvurugana na maofisa wa polisi.
Jana Jumamosi, Maguire alitarajiwa kupelekwa Syros kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo. Beki huyo amefunguliwa kesi ya kuwafanyia fujo maofisa wa polisi pamoja na kujaribu kutoa rushwa. Kesi hiyo ilithibitishwa na Mahakama ya Ugiriki, juzi Ijumaa.
Beki huyo alikwenda nchini Ugiriki na mchumba wake, Fern Hwakins, kwa ajili ya mapumziko baada ya kumaliza msimu wa 2019/20 ambapo alikamatwa katika baa ya Fabrica, juzi Ijumaa.
Ofisa wa polisi mmoja wa Ugiriki, Pretros Vassilakis, alisema: “Walikuwa katika makundi mawili, wakaanza kuwatukana maofisa wa polisi, kwenye kundi hilo walikuwepo watu wenye umri kuanzia miaka 27, 28 na 29.
“Kati yao, watatu walikamatwa wakati tukipambana nao pamoja na huyo mchezaji alimpiga polisi na kumuangusha. Siwezi kusema yale ambayo walikuwa wakituambia kwani hayakuwa maneno mazuri, tukawaweka ndani pale Mykonos.”
Kasheshe
ReplyDelete