August 23, 2020

 



IMERIPOTIWA kuwa, kocha mpya wa Barcelona, Ronald Koeman, amewafungulia njia ya kutokea mastaa watatu wakubwa wa timu hiyo ambao ni Luis Suarez, Sergio Busquets na Jordi Alba.

 

Koeman ametua Barca hivi karibuni akitokea timu ya Taifa ya Uholanzi akichukua nafasi ya Quique Setien.


Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, kwa sasa anajipanga kupata timu ya ushindani huku akisema kuna baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza hawapaswi kuguswa katika mpango wa kuondolewa.


Wachezaji hao ni pamoja Lionel Messi, Marc-Andre ter Stegen. Frenkie de Jong, Clement Lenglet na Nelson Semedo, huku Antoine Griezmann na Ousmane Dembele wakipewa nafasi nyingine ya kuonyesha ubora wao.


Imeelezwa kuwa Koeman pia anataka kuendelea kufanya kazi na beki mkongwe wa timu hiyo, Gerard Pique kwani ni mhimili mkubwa kwenye ulinzi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic