ZLATKO Krmpotić kwa sasa ndiye Kocha Mkuu wa Yanga ametua leo mapema akitokea nchini Serbia kuchukua nafasi ya Mbelgiji, Luc Eymael aliyetimuliwa Julai 27.
Yanga imemchukua kocha huyo akitokea Polokwane City ya nchini Afrika Kusini huku akiwa amefundisha baadhi ya klabu kama APR (Rwanda), Zesco United (Zambia) na TP Mazembe (DR Congo).
Timu hiyo imemchukua kocha huyo baada ya Mrundi, Cedric Kaze aliyekuwa anafundisha Academy ya Barcelona kupata matatizo ya kifamilia.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema :- “Baada ya dili kufeli, haraka tukahamia kwa Zlatko ambaye yeye alikuwa chaguo letu la pili kati ya makocha hao walioleta CV zao Yanga, hivyo kamati ikachukua maamuzi ya kumpitisha Mserbia huyo kuja kuifundisha Yanga,
“Uzoefu wa Zlatko wa kufundisha timu za Afrika ndiyo umetushawishi sisi viongozi kumpa nafasi ya kuja kuifundisha Yanga, kwani aliwahi kuzifundisha klabu za TP Mazembe, Zesco na Polokwane, kocha huyo tumemuachia nafasi mbili za usajili za wachezaji wa kigeni ambazo kama akihitaji mchezaji wake atakayetaka kufanya naye kazi tumsajili,” amesema Hersi.
Amewahi kuwa kocha bora kule DR Congo msimu wa 2016-2017, msimu uliofuata pia akawa kocha bora kwenye Ligi ya Zambia akiwa na Klabu ya Zesco pia akawa kocha bora Afrika. Mwaka 2018 baada ya kutua Botswana kuinoa Jwaneng Galaxy aliibuka pia kocha bora wa msimu.
"Msaidizi ni Juma Mwambusi ambaye ni mzawa na ni pendekezo la kocha mpya kwamba alitaka kufanya kazi na mzawa.
“Pia, kocha wetu mpya wa makipa ni Niyonkuru (Vladimir) ambaye ni raia wa Burundi yupo tayari nchini kwa kufanya kazi yake hiyo, tumeliboresha benchi letu la ufundi kwa ajili ya kufi kia malengo yetu,” alisema Hersi.
na mwaka 2019-20 kocha wa vibonde wa ligi South Africa
ReplyDelete2017 TP Mazembe Congo
2018 Zesco Zambia
2018 Jwaneng Botswana
2019 APR Rwanda
2019-20 Polokwane SA
huyo kocha ni bandika bandua na kwa wale mashabili Eymael aliwaita mbumbumbu na majina mengine.... yetu macho
mbona umeanza mbali sana. huyo kocha kuanzia 2013 kila mwaka anakuwa timu nyingine wakati mwingine katika mwaka mmoja timu anakuwa timu mbili.Halafu hao mbumbumbu na gongowazi wamempa miaka miwili ...mwana kulitafuta mwana kulipata
DeleteNa hiyo Congo kwa TP Mazembe alikuwa assistant ....sasa hiyo honours ya kocha bora aliipataje huku akiwa assistant
ReplyDelete😂😂😂😂 hakuna kocha hapo vichekesho kwa GONGOWAZI aka vyura aka kandambili
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteNyie WE...KUNDU wa Msimbazi mbona mnawashwawashwa sana tuacheni na mambo yetu,hebu wekeni CV ya kwenu hapa tuione inasomekaje halafu tujadili
ReplyDeleteWanateseka kwel
Deletejenga hoja na sio matusi..wengi wanatambua ukivunja neno wekundu sehemu ulipolivunja wewe unapata maneno mawili tofauti na moja wapo ni tusi..au ndiyo wale Eymael alitujulisha kazi yao.
Deletejenga hoja ingia google tafuta rekodi za Sven weka hapo.Ukweli upo na haufichiki...Sasa huyo kocha mpya tangu 2013 kila mwaka una timu yake..kweli ataweka rekodi endapo atamaliza miwili aliyogawiwa na Yanga
Usajili unafungwa tr. 31.8.2020 leo ni 29.8.2020, huu muda utatosha kweli kusajili wachezaji wawili tena wa kigeni?
ReplyDelete....nyuma mwiko
ReplyDeleteIla pimbi wanapenda kuingilia ya watu! Ndo maana mlivyojieungua mkajiita QUEENS! Wanaume mkajiita vile! Ndo maana Mambo yenu ya kiqueen! Mnyama
ReplyDeleteMara zote Queens akicheza na gongowazi princess huwa princess anachezea kichapo tu cha wale wanyama aloita Eymael.
ReplyDelete2019 Mechi ya kwanza Simba Queens 5 na Yanga Princess 1 na ya pili Simba Queens 7 Yanga Princess 0
2020 Simba Queens 3 Yanga Princess 1 na mechi ya pili Simba Queens 5 Yanga princess 1
Ukweli upo!
Kocha wa Wananchi, Kwann mikia wanateseka?
ReplyDeleteShughuli sio yenu mind your business
Hata mie nawashangaa, badala ya kushughulika na kikosi Chao kilichojaa wastaafu, wanahangaika na jeshi la vijana wa Jangwani
DeleteMajibu ya CAS bado?Mtandao wa FIFA unaonyesha Morrison mchezaji wa Simba. Kweli hizo milioni 600 tutazipata?Au danganya toto kwa sisi wanachama na mashabiki.
ReplyDeleteNdugu, wewe umeona huo mtandao wa FIFA unaoonesha Morrison mchezaji wa Simba? Usipumbazwe na propaganda za Mikia FC wanaosubiri mchezaji atakiwe na Yanga wao ndo wamwone, kama fisi anayesubiri kubakiziwa
DeleteMlisema Morrison ni mchezaji wenu Sasa hizo nafasi mbili zimetoka wapi?
ReplyDelete