August 29, 2020


 FELIX Minziro maarufu kama Baba Isaya, leo Agosti 29 ametambulishwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Geita Gold.


Amesaini dili la mwaka mmoja kwa ajili ya kukiongoza kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kupanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.


Imepambana mara mbili mfululizo Geita kupanda Ligi Kuu Bara ila ilikuwa inaishia hatua ya playoffs kwa kupoteza mechi zake ambapo msimu wa 2019/20 ilifungwa na Mbeya City. 


Minziro alikuwa Kocha Mkuu ndani ya Klabu ya Mbao FC ambayo itashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kuangukia pua Kwenye mchezo wa playoffs dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya msimu wa 2019/20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic