UONGOZI wa Azam FC umeweka bayana kuwa kinachochelewesha dili la kiungo Salum Abubakar kumalizana na Yanga ni suala la dau ambalo Yanga wamelitoa kwa Azam FC.
Habari
zinaeleza kuwa Yanga wanahitaji saini ya Sureboy ili awe mbadala wa Papy
Tshishimbi aliyeachwa mazima ndani ya kikosi hicho ila walipeleka dau la
milioni 20 kwa Azam FC jambo lililochelewesha kiungo huyo kuibukia Azam FC.
“Sureboy ana
mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC, yeye mwenyewe amesema anahitaji changamoto
mpya ila dau walilopeleka Yanga kwa Azam FC ni milioni 20 jambo ambalo
limechelewesha dili la kiungo huyo,” ilieleza taarifa hiyo.
Abdulkarim
Amin, Mtendaji Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wamepokea ofa kutoka kwa Yanga
ambao wameonesha nia ya kumtaka kiungo huyo watawajibu mapema ili kufanya nao
biashara.
“Barua ya
mwanzo walikuwa wanauliza kama wanaweza kumpata mchezaji huyo tukawajibu kuwa
bado ana mkataba wa mwaka mmoja, Agosti 6 walileta rasmi barua ya kuomba
kumpata mchezaji wetu jambo ambalo tunalifanyia kazi ili tufanye nao biashara.
“Tukipata bei ambayo ni sahihi kwetu tunamruhusu kwa kuwa mchezaji mwenyewe ameonyesha nia kutaka kuondoka. Ikumbukwe kuwa wakati ule walipokuwa wakimhitaji Nchimbi, ofa ya kwanza ilikuwa ndogo baadaye wakaongeza ofa tukamuuza mpaka sasa wapo naye hata kwa huyu pia hatuwezi kushindwana,” amesema.
viongozi wangu kuna tatizo gani, kila mchezaji dau dogo akina yondani na Abdul tatizo pia dau dogo
ReplyDelete