MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa yupo tayari kubeba mikoba ya Luc Eymael ambaye amefutwa kazi ndani ya jangwani ikiwa mazungumzo yatakwenda sawa.
Eymael, raia wa Ubelgiji alifutwa kazi jumla ndani ya Yanga, Julai 27 baada ya kuongea maneno yaliyokuwa yakiashiria ubaguzi wa rangi kwa mashabiki pamoja na kusema kuwa hafurahishwi na mashabiki wa hapa kwa kuwa hajui soka.
Akizungumza na Spoti Xtra, Maxime ambaye amekuwa imara katika kukiongoza kikosi cha Kagera Sugar ndani ya msimu wa 2019/20 baada ya kumaliza kikiwa nafasi ya nane na pointi 52 alisema kuwa yupo tayari kufanya kazi ndani ya Yanga.
“Mimi nipo Kagera Sugar kwa sasa ndipo ambapo ninafundisha, ikitokea Yanga wakahitaji kupata huduma yangu ni suala la mazungumzo, sina tatizo ikiwa kila kitu kitakuwa sawa nitafanya kazi pale, timu yoyote ile ambayo inahitaji huduma yangu ninaweza kufanya nao kazi,” alisema Maxime.
Spoti Xtra lilimtafuta Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ambaye alisema kuwa:”Nipo kwenye kikao kwa sasa.”
Uongozi wa Kagera Sugar walishalitolea ufafanuzi suala la kocha kuondoka hapo na kuwa hawana mpango wa kumwachia. Bado ni kocha wao na atandelea na kukinoa kikosi cha Kagera Sugar
ReplyDeletemtu kaongea mwenyewe wewe unaleta maneno ya kwenye kanga unaeza shindana na hela weye
DeleteHakuna mikataba isiyovunjika kwenye soka. Anaweza ondoka muda wowote akitengewa pesa tu mkataba unavunjwa na anasepa
ReplyDelete