August 10, 2020

 NYOTA saba ambao walikuwa ndani ya kikosi cha Yanga wamepewa mkono wa kwaheri baada ya dirisha la usajili kufunguliwa Agosti Mosi na mambo yanaendelea mpaka Agosti 31.

 

Yanga ikiwa imefunga mabao 45 wamehusika kwenye kufunga mabao 18 huku wakitengeneza jumla ya pasi sita za mabao na kuwafanya mchango wao kuhusika kwenye jumla ya mabao 24.

 

Labda kama wasingetimiza majukumu yao habari ingekuwa nyingine, kwa kuwa maisha lazima yaendelee acha tusubiri msimu ujao maingizo mapya mambo yatakuaje.


Tayari vurugu za usajili zimeanza kibabe kwa Yanga kama kawaida wakipigana vikumbo na watani zao Simba pia na mshindani wao mwingine ni Azam FC.

 

Wazir Junior, mshambuliaji kutoka Mbao FC, Bakari Mwamnyeto beki kutoka Coastal Union, Yassin Mustapha naye ni beki kutoka Polisi Tanzania, kiungo mkabaji Zawadi Mauya aliyekuwa akikipiga Kagera Sugar, Kibwana Shomari beki kutoka Mtibwa Sugar na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ni usajili wa mwanzo.

 

Huu hapa mchango wa nyota saba ambao wamepigwa chini mazima baada ya dili zao kufika tamati, takwimu ni za ligi kuu msimu wa 2019/20 kama ifuatavyo.

PAPY TSHISHIMBI


Amecheza jumla ya mechi 23 na kutumia dakika 1,936 kati ya 38 akikosekana kwenye mechi 16. Ana pasi moja ya bao ndani ya ligi.

 

Hizi hapa mechi zake.Ruvu Shooting (90), Mbao FC (90), JKT Tanzania (90), Mbeya City (90), KMC (90), Prisons (26), Biashara United (20), Ndanda (90), Alliance (90), Simba (90), Azam FC (90), Singida United (90), Mtibwa Sugar (90), Lipuli (90), Ruvu Shooting (90), Mbeya City (90), Prisons (90), Polisi Tanzania (90). Coastal Union (90), Mbao (90), Simba (90), KMC (90), Namungo (90).

 

DAVID MOLINGA


Amecheza jumla ya mechi 32 kati ya 38 akitumia jumla ya dakika 2,104 ndani ya Yanga.Mechi 27 ameanza kikosi cha kwanza mechi tano ameanzia benchi.


Ametupia mabao 11 na kutoa pasi moja ya bao. Hizi hapa mechi na dakika zake uwanjani.Polisi Tanzania (dk 90), JKT Tanzania (dk 60), Alliance FC (dk 90), Ruvu Shooting (dk 90), Coastal Union (dk 90), Mbao FC (dk 74), Ndanda (dk 90), KMC (dk 90), Mbeya City (dk 90), Tanzania Prisons (dk 90), Biashara United (dk 45), Azam FC (dk 90).


Nyingine ni mbele ya Singida United (dk 67), Mtibwa Sugar (dk 68), Lipuli (dk 29), Ruvu Shooting (dk 68), Mbeya City (dk 64), Prisons (dk 30), Mbao (dk 63), KMC (24), Mwadui FC (dk1), JKT Tanzania, (dk11), Azam FC,(64), Ndanda, (78), Ndanda,(78), Biashara United (dk90).Kagera Sugar (dk 90), Singida United (dk 60), Mwadui (dk 60), Mtibwa Sugar (dk 57), Lipuli (dk 80).

 

JAFFARY MOHAMED


Amecheza mechi 19 kati ya 38 ambazo Yanga wamecheza msimu ulioisha.Hizi hapa mechi alizocheza:- Ndanda FC, JKT Tanzania, Alliance, KMC, Mbeya City, Tanzania Prisons, Ndanda, KMC, Mbeya City, Tanzania Prisons, Azam FC, Singida United, Mtibwa Sugar, Lipuli, Ruvu Shooting, Mwadui, Polisi Tanzania, Simba, Azam FC.

 

TARIQ SEIF

 

Nyota huyu aliibuka ndani ya Klabu ya Yanga akitokea nchini Misri kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa mchezaji huru.Ndani ya Ligi Kuu Bara amefunga jumla ya mabao matatu, bao lake la kwanza ilikuwa Uwanja wa Taifa mbele ya Biashara United na ana pasi moja ya bao alianza kwenye mechi tatu tu tangu ajiunge na kikosi hicho.

 

DANTE

Andrew Vincent ‘Dante’ hakuwa na msimu mzuri ndani ya Yanga kwa kuwa alikuwa kwenye mgogoro na uongozi kwenye suala la maslahi jambo lililomfanya agome kurejea kikosini.Aliporejea kikosini alijenga ushkaji na benchi huku akisema kuwa hakuwa anajua sababu ya kutopewa nafasi ya kucheza.

 

MOHAMED ISSA ’BANKA’

Ameanza kikosi cha kwanza kwenye jumla ya mechi tatu ndani ya ligi ambazo ni dhidi ya Simba, Kagera Sugar na Mbao FC. Anatajwa kuwa mbioni kutua Azam FC.

 

MRISHO NGASSA

Kiungo huyu mshambuliaji mkongwe ndani ya ligi kuu mwishoni alikuwa amewaka baada ya kuwa kwenye ubora wake. Ametupia jumla ya mabao manne msimu wa 2019/20 na kutoa pasi tatu za mabao.Ameanza kikosi cha kwanza mechi nane ilikuwa ni mbele ya; Polisi Tanzania, Coastal Union, Mbao FC, Biashara United, Polisi Tanzania, Kagera Sugar, Mwadui na Lipuli

 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic