August 24, 2020

 


KLABU ya Yanga leo Agosti 24 imemtambulisha rasmi aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa kuwa mshauri wao.

Senzo atashirikiana na uongozi wa klabu na kampuni ya GSM kwenye mazungumzo ya mabadiliko ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo wakishirikiana na watu wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) na Klabu ya Sevilla ya Hispania, kuanza mchakato mzima.

 

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, amemtambulisha Senzo mbele ya wanahabari na kusema kuwa sasa kazi ya kuubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo unaanza rasmi.

 

“Yanga SC tumemchukua Senzo kama mshauri wetu hasa kwenye haya mabadiliko tunayokwenda kuyafanya. Tunao washauri wa La Liga na Sevilla, tumeona na yeye tumuongeze sababu ana rekodi nzuri ya uongozi wa masuala ya soka, na ameshaanza kushiriki vikao vyetu,” amesema.

 

Senzo amesema;“Si kazi rahisi kujiunga na Yanga kwa sababu ni moja ya klabu kongwe, kubwa na yenye historia nzuri barani Afrika. Kwangu ni bahati, nitafanya kazi ya kuishauri klabu na kuhakikisha tunaingia kwenye mfumo mpya, wa kisasa kuiongoza klabu ili kuwa tayari kushindana.

 

“Nitakuwa mshauri na kiunganishi kati ya La Liga na Sevilla pamoja na Yanga, nitatoa ushirikiano wangu wote kwa kushirikiana na viongozi wa klabu pamoja na GSM kuleta mafanikio ndani ya klabu, hivyo sasa najisikia mwanafamilia wa Yanga ,” amesema.


Senzo ameibukia Yanga akitokea Simba, Agosti 9 muda mfupi baada ya kutangaza kubwaga manyanga ndani ya Simba.

13 COMMENTS:

  1. Lakini mwandishi, ni lazima useme Senzo wa Simba?
    Kila ukiandika habari ya Senzo lazima umtaje Mnyama! Naona Kama ni chokochoko vile!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hatujaona akiandika Bernard Morrison wa Yanga aanza kuichezea Simba

      Delete
    2. Mwandishi hana weledi kabisa yawezekana ni kanjanja. Kwanza hii anaidhalilisha Yanga zaidi kuliko hata Simba.

      Delete
    3. Kwan ukitaja morrison si lazma useme alitokea Yanga!?

      Delete
  2. Si kama mnavyomtaja Morrison tu? Ukitajwa unaumia nini?

    ReplyDelete
  3. Kazi unayoenda kuifanya bwana senzo ni ngumu sana, kwa sababu ushauri sio amri unaweza kumshauri mtu zaidi ya mara tatu halafu hafuati ushauri wako sijui unajisikiaje.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na ndicho kilichomuondoa Simba,baadhi ya ushauri wake ulikuwa hauzingatiwi badala yake Haji Manara ndo amekuwa mwenye sauti mbele ya tajiri

      Delete
  4. Mpaka sasa anatumia vibali vya simba vya kukaa na kufanyia kazi ila iwa sababu manyani uneducated hamuwexi kuelewa

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe ndiyo mkewe??mbona unzijua siri za ndani sana tuambie tu kama wewe ndiyo shemeji yetu kwa Senzo

      Delete
  5. Simba please mi siwaiti mikia sawa mmefanya mabadiliko tuache hisa za mo ,je ile asilimia yenu mnaigawaje? tusaidie sisi Mbumbu Wananchi mnaotuita Manyani hili napo tuige kwenu Kama tulivyo mchukueni masingiza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka hapa umenena na kiukweli sidhani kama kuna mshabiki anaweza kulijua hili ila tuseme ukweli tu kuwa sisi mashabiki tupo gizani ila kwa kuwa masuala ya pesa kama shabiki yamhusu maana sisi tunafurahi mafanikio ndo maana utaona club ikiuza mchezaji tegemeo halafu sisi tutagombana sana pengne kuna anguko la uchumi lakini mshabiki hajui hilo hata kidogo

      Delete
  6. Na pia afanikishe mchango wa mastraika wawili wakigeni

    ReplyDelete
  7. Mo ana asilimia yake na ya kwenu vipi? Maana Wengine mnajua hata Senzo tabasamu lake lkn yenu hamjui bila kusahau ya Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic