August 31, 2020


 YANGA jana Agosti 30 Uwanja wa Mkapa ilihitimisha kilele cha wiki ya  Mwananchi kwa ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Klabu ya Aigle Noir ya Burundi.

Mchezo huo ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Mkapa ulikuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho kwa timu zote kucheza mpira wa darasani na mipango mingi ndani ya uwanja.

Yanga ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 38 kupitia kwa ingizo jipya ndani ya kikosi hicho Tuisila Kisinda akimaliza pasi ya nyota mzawa Feisal Salum ambaye alikuwa ni nyota wa mchezo wa jana.

Aigle walimaliza wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao mmoja Koffi Kuassi kuonyesha kadi nyekundu dakika ya 40 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano dakika ya 10 na ile ya pili ikamfanya mwamuzi asiwe na chaguzo zaidi ya kumuonyesha kadi nyekundu kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

Licha ya wapinzani hao wa Yanga kuwa pungufu bado waliendelea kuwa imara kwa kucheza kwa utulivu huku mipango yao mingi ikiishia miguuni mwa Bakari Mwamnyeto beki mpya wa Yanga aliyesaini dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Coastal Union.

Bao la pili kwa Yanga lilipachikwa na mshambuliaji mpya tena wa Yanga, Michael Sarpong ambaye alimaliza kazi ya pasi ya Ditram Nchimbi dakika ya 52 kwa kupiga kichwa kilichozama moja kwa moja nyavuni.  

Winga wa Yanga, Farid Mussa amesema kuwa walipambana mwanzo mwisho kwa kuwa walikuwa wanajua wanachotaka huku akiwaomba mashabiki wawape sapoti.

Muangola wa Yanga, Carlos Carlinhos aliingia dakika ya 81 akichukua nafasi ya beki Abdalah Shaibu,'Ninja' na alifanya jaribio moja ambalo halikuzaa matunda.

Wengi walifurahia pia show ya kibabe iliyofanywa na Harmonize, Konde Boy ambaye aliingia kwa mtindo wa kininja uwanjani kwa kutumia kamba ndefu jambo lililwafanya mashabiki wengi wamshangilile mwanzo mwisho.


Licha ya Konde Boy kuanguka wakati wa kushuka uwanjani alionyesha kwamba yeye ni mwamba na yupo imara kwa kufanya onyesho ambalo lilikonga nyoyo za mashabiki wa Yanga pamoja na wadau ambao walifuatilia onyesho hilo lililorushwa mubashara Azam Tv.


Yanga inajiaanda kwa sasa na mchezo wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Septemba 6 Uwanja wa Mkapa itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons.

14 COMMENTS:

  1. Mchezaji wa Aegle Noir alipewa kadi nyekundu dakika ya 28, wala sio dakika ya 40 kama mwandishi alivyoandika. Wamecheza pungufu muda mwingi jamaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Basi tufanye draw match. Muhimu hawakununua match. Walioshinda 6-0 tusubiri na UD Songo

      Delete
    2. Sawa Simba ilitolewa na UD Songo kwa UD faida ya UD Songo kupata goli la ugenini!
      Je umesahau Yanga ilivyoaga mashindano ya CAF?ni laana ndiyo inaweza kuwa sababu..Abdul Aziz Makame aliwafungia Zesco..Je
      makame ni mchezaji wa Zesco?...Chance ya kucheza CAF iliipatikana baada ya Simba kuwa imefanya vizuri na jumla ya timu za Tanzania kuongezwa toka 2 hadi 4...ndiyo Yanga ikaweza shiriki mashindano hayo.Hivyo usiwabeze Simba kutolewa na UD Songo...Yanga walijitoa wenyewe kwa kujifunga goli dak ya 78!

      Delete
  2. Ni kweli goli la kwanza lilifungwa dk 38 wakiwa pungufu huyu mwandishi analake jambo

    ReplyDelete
  3. Ok basi mechi irudiwe hii siyo Vitalo Buana

    ReplyDelete
  4. Waandishi wanawapaka rangi tusubiri October 18

    ReplyDelete
    Replies
    1. Akili fupi utazijua tu badala ya kujipanga kwa club bingwa atii tusubiri...yaani akili yako mwisho buza

      Delete
  5. Kadi ya kwanza kapewa dakk 28 ya pili kapewa dakk 40 na yanga ikiw tayar inaongoza goli moja.

    ReplyDelete
  6. red kadi imetolewa dak ya 28..hadi red card imetolewa ndiyo Yanga wameanza kushinda..
    kipindi cha pili substitution imefanyika baada ya goli la pili kupatikana..na walioingia substitution hakuna hata mmoja aliyefunga bao...ki uhalisia hakuna kikosi cha pili Yanga

    ReplyDelete
  7. Hahahaha kweli nyumbu fc hata wawakaange watabaki na unyumbu, sasa badala ujipange na CAF CHAMPIONS LEAGUE yanakomalia tarehe 18, nasubiri msimu huu mtapigwa 10-0

    ReplyDelete
    Replies
    1. ipi bora kufungwa na hizo timu huko kwao bao tano...bado ukaingia makundi

      au kupata chance ya nadra ukacheza CAF kisha ukajifunga ili timu unayocheza nayo isonge mbele..

      msijifanye mnaijua sana CAF kana kwamba Yanga ilikuwa ikicheza kila mwaka wakati wa Malinzi lakini ni madudu tu? 2018 bao nne na US Algiers na Dar pia wakawafunga..Gor Mahia waliwapiga 3 Nairobi na Dar pia wakawafunga..Ni kwa Ryon tu ndiyo Yanga ilipata bahati...
      Narudia bora tano wakija hapa Dar hata ukiwafunga moja kuliko Wale wanaojifungisha wenyewe

      Delete
  8. Tutawafunga mdomo tena kwa kipigo cha mbwa mwizi.Vitalo wamekula Yanga + 2,Namungo wakala Yanga -2,AFC wakala Yanga + 2,mjipange msilie na marefa maana ndio zenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic