ABDULHAMAN Humud maarufu kama Gaucho nyota mpya ndani ya Klabu ya Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo wa kirafiki dhidi ya Azam FC.
Humud amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar anacheza nafasi ya kiungo.
Nyota huyo amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya ushindani kwani maandalizi na mazoezi tumefanya kiasi cha kutosha tuna amini kwamba mchezo utakuwa mzuri na wenye ushindani mkubwa.
"Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na kushuhudia ushindani ndani ya uwanja," amesema.
Azam FC leo ni kilele cha Azam Festival ambapo kwa sasa mechi za utangulizi zimeanza viwanja vya Azam Complex.
0 COMMENTS:
Post a Comment