August 6, 2020

IMEELEZWA kuwa sababu kubwa ya uongozi wa Yanga kuachana jumla na mabeki wao wawili wakongwe Kelvin Yondani na Juma Abdul ni kushindwa kufikiana makubaliano katika suala la kusaini dili jipya.

Abdul na Yondani Agosti 5 jana waliachana na Yanga baada ya kuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba wao. 

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa wachezaji hao amesema kuwa:"Yanga walikuwa na mpango kwenye mpango wa kuwapa dili mabeki hao ila wameshindwana kwenye mpango wa malipo, uongozi wa Yanga ulikuwa tayari kuwapa mikatba mipya bila fedha za usajili jambo ambalo lilipokelewa tofauti kwa wakongwe hao na kuamua kuondoka ndani ya Yanga," ilieleza taarifa hiyo.

Abdul ndani ya Yanga alikuwa ni nahodha msaidizi na kwa msimu wa 2019/20 amehusika kwenye jumla ya  mabao 6 kati ya 45 yaliyofungwa na Yanga akiwa ametoa pasi sita zilizoleta mabao.

Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 ndani ya Ligi Kuu Bara, Abdul alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi 28.

Yondani yeye ameanza kwenye jumla ya mechi 22 kwenye kikosi cha kwanza kwa msimu wa 2019/20.

Abdul amesema:"Ninadhani msimu ujao sitakuwa ndani ya kikosi kwa kuwa tumeshindwana kwenye makubaliano."

4 COMMENTS:

  1. Do kusema wanasajili kwa mali kauli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani lazima acheze Yanga,au ndo uchochoro wenu ,hataki mwambie aje kwenu Kama Ajibu si mnazo za Ame Ali

      Delete
  2. KWA MTINDO HUO SIYO HAKI KABISA WAKONGWE KAMA HAO KUACHWA ILIBIDI BUSARA ITUMIKE YANGA INAENDA KUBAYA, YALE YALE YA 2019 YATAENDA KUTOKEA

    ReplyDelete
  3. SUBIRINI VIONGOZI WAMALIZE KAZI KILA KITU KITAKUA WAZI NA HAPO NDIPO MTAWAHUKUMU VIONGOZI PALE MTAKAPOONA WAMEKOSEA AMA KUSEMA SASA HIVI NI KAMA KUWAVURUGA TU

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic