Chama ameshatwaa tuzo mbili ikiwa ni ile tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho pamoja na tuzo ya mchezaji bora ndani ya Simba iliyotolewa na mdhamini mkuu wa timu hiyo SportPesa.
Kwa sasa anawania tuzo mbili ndani ya Ligi Kuu Bara ambazo ni ile ya mchezaji bora akipambana na Nicolas Wadada wa Azam FC na Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union na kiungo bora ndani ya VPL akipambana na Lukas Kikoti wa Namungo FC na Mapinduzi Balama wa Yanga.
Haji Manara Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa Chama ana vigezo vya kubeba kila tuzo kwa kuwa uwezo wake unaonekana na rekodi zinambeba.
Jumla Chama amefunga mabao sita na pasi 13 akiwa amefunga mabao mawili ndani ya ligi na mabao manne kwenye Kombe la Shirikisho, pasi 10 ni kwenye ligi na tatu ni za Shirikisho.
Sherehe za tuzo za Ligi Kuu Bara zinatarajiwa kufanyika Agosti 7,2020 katika ukumbi wa Mlimani City.
0 COMMENTS:
Post a Comment