August 24, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utafanya kazi kwa ushirikiano na aliyekuwa Mtendaji Mkuu ndani ya Klabu ya Simba, Senzo Mbatha kwa kuwa ni mtu mwenye uzoefu na masuala ya mpira.


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, leo Agosti 24, makao makuu ya Yanga, Mwenyekiti wa timu hiyo, Mshindo Msolla amesema kuwa wanaamini wapo na mtu sahihi katika masuala ya ushauri ndani ya klabu hiyo.

"Tupo kwenye mabadiliko ambayo tayari tumeshaanza tukishirikiana na watu wa La Liga hivyo kikubwa ambacho tunakifanya ni kuwa na watu sahihi ambao watatupeleka kwenye mafanikio.

"Kwa sasa tunafanya kazi pia na Senzo ambaye ana uwezo mkubwa kwenye masuala ya michezo, tayari kwenye vikao vyetu vya La Liga ameanza kutoa mchango wake hivyo tua amini tupo na mtu sahihi," amesema.

Senzo amesema:"Nitafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na viongozi wa Yanga ikiwa ni pamoja na mwenyekiti pamoja na viongozi wengine wote kwa kuwa ninatambua majukumu yangu na kazi yangu pia.

"Kikubwa ni kusimama katika ukweli na uwazi ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea," amesema.

Agosti 9, Yanga ilimalizana na Senzo Mbathha muda mfupi baada ya kutangaza kujiuzulu ndani ya Simba


7 COMMENTS:

  1. Mbonaa lile tabasamu tulilolizoea la Senzo limepoteaa ghafla au ndio nafsi inamsutaaa???
    Hii ndio Bongoland buana awe na amani tuu na anatakiwa kila la kheri huko alipo!

    ReplyDelete
  2. Timu ikianza Kuchapwa na baadhi ya wachezaji aliohusishwa nae kutoonesha kiwango ndipo atapoikumbuka Simba

    ReplyDelete
  3. Kakosea mlango wa kutokea timu inaomba mchango kwa mama ntilie ili usajili wachezaji itakapofika muda wa mishahara itakuweje na huyo Senzo siatakimbia na kutelekeza timu emb Yanga tuwe makini na masuala ya utunzaji wa wachezaji tusije anza kulaumiana badaye timu ikipoteana.

    ReplyDelete
  4. Hivi Yanga wameshindwa kupata jina la cheo cha Senzo? Mara aitwe "Senzo wa Simba" au "Aliyekuwa mtendaji mkuu wa Simba"!!! Viongozi kuweni serious na mambo mnayofanya msitawaliwe na mihemuko.

    ReplyDelete
  5. Nam...Kwan walioita Senzo wa Simba ni Yanga au mwandishi aliyeandika Makala??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimegunduwa ni mwandishi maana habari na picha hiyohiyo nimeiona Mungwana lakini wamemwandika jina lake na kazi atakayofanya. Hapa kunatatizo la weledi wa mwandishi wa hizi habari.

      Delete
  6. Mshindo Msola anataka kutuvurugia usajili. Ana malengo gani huyu??! Mimi huwa simuelewi na wakati mwingine nakuwa na mashaka naye. Benchi la ufundi liliomba wasajiliwe wachezaji wanane kwanza wa kigeni katika hili dirisha kubwa la usajili, ili likitikea pengo au kuna mchezaji kashindwa kwenda na rhythm ya timu tumalizie nafasi mbili zilizobaki katika dirisha dogo.
    Kwa nini huyu mzee anang'ang'aniza wasajiliwe wachezaji kumi wakati huu?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic