JOTO la mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Namungo, limepanda ambapo leo Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, moto utawaka wakati timu hizo zikipambana.
Simba na Namungo zinatarajia kufungua pazia la msimu wa 2020/21 kwa kucheza mechi hiyo ambapo baada ya hapo, Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, juzi Ijumaa usiku walifika jijini Arusha wakitokea Dar kwa ajili ya mchezo huo, huku Namungo nayo ikifika siku hiyohiyo.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alisema: “Tupo tayari na kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa Ngao ya Jamii.
Kocha wa Namungo, Hitimana Thiery, amesema:
“Tumejipanga kwa ajili ya mchezo huo, tumefika huku kwa kuchelewa sana, tuliingia jana (juzi) usiku, sehemu tuliyofikia haikuwa yenye mazingira mazuri, ikabidi tuhame na kutafuta sehemu bora.
“Kwa namna ninavyoona, siwezi kusema moja kwa moja kwamba tunaweza kushinda mechi hii. Mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa 9:30 alasiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment