August 25, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambayo inatarajiwa kupigwa Oktoba 18, Uwanja wa Mkapa imepangwa mapema sana jambo ambalo linawapa hasira ya kujipanga vizuri.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa alipoona ratiba alishangaa kwa kuwa wao wameshakiweka kikosi tayari na wapo tayari kwa ushindani huku akisisitiza kuwa wapinzani wao hao watakutana na balaa la nyota kama Larry Bwalya na Luis Miquissone.

 

“Wale wenzetu tunakutana nao Oktoba 18 mwaka huu kwenye ligi, dah! Itakuwa balaa, mbona wametufanya tukutane mapema, yaani sijui itakuwaje, maana hilo mbungi litakalopigwa siyo la nchi hii.

 

“Fikiria una mtu kama Bwalya (Larry), Miquissone (Luis), Chama (Clatous) hapo ujue wengine sijawataja mimi sijui itakuwaje, ila tusubiri na tuone,” alisema Manara.


Bwalya ni ingizo jipya ndani ya Klabu ya Simba alitambulishwa rasmi siku ya kilele cha Simba, Agosti 22, wakati wakicheza dhidi ya Vital'O ya Burundi ambapo Simba ilishinda mabao 6-0 huku yeye akitoa pasi moja ya bao Uwanja wa Mkapa.

12 COMMENTS:

  1. Manara usitupe kiwewe. Wewe subiri tupate hela ya bakuli ambayo sisi wanachama kwa hiari ya mapenzi yetu tumeamuwa kuichangia Yanga yetu ili wapatikane Hao wawili wataoikata mikia yenu halafu tena ndio mtapokaa sawa na kuufyata

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mikia kesha wakata Mo kwa kuwabadilishia nembo, kifuatacho ni kuweka dengu na pilipili.

      Delete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. kuna fununu Tusyusenge kutoka Angola anakuja yanga. jamaa nzuri kweli kwa kupachika mabao.

    ReplyDelete
  4. Bwalya au Shiboub maana mwaka Jana Simba day Ali Uzidane mpira lkn yupo wapi?Mimi nilichoona kipya kwenye usajili wa Simba ni Morisson , Wengine na Ndemla sawa tu kwa maono na uelewa wangu

    ReplyDelete
  5. Bwalya Kama Ligi hamtaivuluga na marefa wenu hasa Dada Zablon and co .Mpira utakuwa mgumu Simba marefa wanaharibu hasa pale hesabu zinapoanza kwendana na Yanga ,juzi mliandika kwamba Morisson ataipa Simba Penalt ni kweli huyo jamaa ktk ubora wake Simba watafaidi ,lkn angebaki Yanga Penalt haitoki labda mtu afe, kumbuka Ligi ilopita tofauti ya Pointi saba Na Simba tilinyimwa Penalt nne hv na hao marefa wa TFF Karia na aliyekuwa anaangushwa ni BM.Tutakumbuka maneno ya Luc Eymael na Zahera kuhusu Simba na TFF

    ReplyDelete
  6. Samahani huyo dada nilo mtaja kila mechi ya Simba lazima awape tuta hata Kama kirafiki na pili mechi Yanga na Mbeya City kwenye ule UtekeleZi jamaa lilimkata Sibomana yule mama akabana,eti TFF wanamfungia kuruhusu mchezo uchezwe Uwanja tope .Lakini kwa akili ya kawaida yule alijua Yanga watapigwa cse Uwanja tope lkn baada ya Yanga kumudu ile hali wakaanza kuwakilishwa Mbeya City akaanza kuharibu

    ReplyDelete
  7. Malalamiko FC mbona mmeanza kulalamika mapema sana? Si mnasema mmesajili vizuri? Subirini muziki.

    ReplyDelete
  8. andikeni malalamiko yote kabla msimu haujaanza

    ReplyDelete
  9. yanga hatuwezi kukwepa kipigo kwa simba wenzetu timu iko na kocha sisi tunaandamana kama vyama vya siasa na mpira ni mbinu tusubiri kipigo cha mbwa mwizi

    ReplyDelete
  10. yanga hatuwez kukwepa kipigo kwa simba hii wenzetu wako na kocha wanafanya maandaliz sisi tunaandama kama vyama vya siasa tusubiri kupihwa 4G

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic