SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC.
Mchezo wa leo, Agosti 30 utakaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.
Sven amesema:"Wachezaji 20 wapo tayari kwa mchezo.Maandalizi ya msimu hayajawa marefu lakini tulikuwa na mechi nzuri za kirafiki ambazo zimekuwa na faida kwetu.
"Nitakosa huduma ya wachezaji wanne kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Luis (Miqussone), Pascal (Wawa),Chriss (Mugalu) na Gerson (Fraga)," amesema Sven.
Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wana imani watapata matokeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment