August 29, 2020


 SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa) ni kama limemaliza utata wa usajili wa mchezaji Bernard Morrison aliyetua Simba huku akiwa na mvutano na klabu yake ya zamani ya Yanga, baada ya mtandao wao wa usajili kuonyesha kuwa ni mali ya Simba.

 

Usajili wa Morrison kutua Simba ulivuta hisia za mashabiki wa pande zote mbili za Simba na Yanga kufuatia suala la kimkataba lililokuwa likimkabili hadi pale maamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kutoa maamuzi ya mchezaji huyo kuwa huru, hivyo kuangukia Simba.


Akizungumza na Championi Ijumaa, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema kuwa, hadi sasa bado anashangazwa na uongozi wa Yanga kuendelea kulalamika juu ya usajili wa Morrison huku mtandao wa Fifa ukiweka wazi kuwa mchezaji huyo ni mali ya Simba.

 

Aidha, aliongeza kuwa iwapo Yanga watahitaji kesi ya Morrison kusikilizwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), watatakiwa kutoa euro 15,000 ambazo ni zaidi ya Sh 40m ndipo suala lao lisikilizwe ikiwa ni kwa jaji mmoja na wakihitaji zaidi itabidi waongeze fedha.


“Suala hili linachekesha kwa sababu, sidhani kama viongozi wa Yanga hawajui sheria, wanaijua vizuri, Morrison alikuwa mchezaji huru, kwenye mtandao wa Fifa inaonyesha amesajiliwa Simba, mtandao huo unajieleza kabisa kuwa msimu wa 2019/20 alikuwa mchezaji wa Yanga na msimu ujao wa 2020/21 ni mchezaji wa Simba. Hii inaonyesha katika sehemu ya uhamisho wa mchezaji.

 

“Sijajua Yanga hadi leo wanacholalamika ni nini kuhusiana na mchezaji huyo, mwenyekiti wa kamati ya hadhi za wachezaji alitamka hadharani kuwa mkataba ule una upungufu, lakini hata wakienda CAS wanaweza wasifanikishe, kwanza siyo kazi nyepesi hadi kufikia kesi kusikilizwa, inaweza kuchukua muda mrefu hata mwaka mmoja kama ilivyokuwa kwa Okwi wakati tunawadai Etoile Du Sahel.

 

“Unatakiwa kuwakilisha dokumenti zote Fifa kisha wao ndio wakupangie jaji ambaye atatakiwa kulipwa euro 15,000 kwa jaji mmoja ambapo pia itategemea kesi inahusu nini na iwapo atatakiwa kuongezwa jaji wa pili ili aweze kusikiliza basi pesa zinaongezeka, hivyo ni vyema waweke risiti hadharani, isije wakatumia muda huu kuwahadaa mashabiki wao,” alisema Rage.

19 COMMENTS:

  1. Mbio za sakafuni huangukia ukingoni. Ni aibu tupu kwa klabu kubwa kama Yanga Mabingwa Wa Jadi kujifikisha wao wenyewe Katika hali kama hii waliokuwanayo hivi sasa. Jee wataendelea bado kutaka walipwe shilingi 600,000,000 ili eti iwe funzo kwa wengine au ndio Simba bado imependekewa na FIFA sijui nani anayewadanganya manaake wamepeleka mashtaka kwa kujiamini kabisa

    ReplyDelete
  2. Viongozi wa utopolo fc wanatabia za bongo movie, wao ni maigizo tu kila cku tatizo lao hawana maadili wala uweledi na maswala ya michezo, tu kutane tarehe 18/10/2020 kwa mkapa stedium trip hii mnakula nyingi sana.

    ReplyDelete
  3. Hilo suala limekwisha, yanga wanazuga tuu

    ReplyDelete
  4. Wangojee sasa kujibu kuhusu saini yao feki waliyomzuluia Morrison kuwa ni saini yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nawe umezaliwa kwa bahati mbaya ndio maana mama yako ana matako meusi fiii

      Delete
  5. Walihadaiwa na waandika magazeti na wakaingia kichwa mbele pamoja na lile dau la milioni Mia sita

    ReplyDelete
  6. Hahaha nashangaa kweli mtu unamfurahia fisadi kama yeye anaakili kuliko viongozi wa yanga kwann alikuwa anafanya madudu kipindi chake cha uongozi pia pesa wanatoa yanga.hatoi yeye achamambo yafanyike kama yalivyopangwa sisi hatuwezi kutishika na maneno ya kwadi wenu huyo ambae kila sehemu hatakiwi siasa imemshinda Moira nao umemshinda

    ReplyDelete
  7. The way kichwa habari kilivyoandikwa nikajua yanga tayari wameshapeleka shauri lao CAS na Majibu yametolewa ila mpaka namaliza kusoma habari sjaona mahali jaji wa CAS ametoa hukumu sasa hii habari inalenga nini labda au ndo waandishi wetu vilaza?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwenye blog na rage bado wanaumia na usajili wa mbuyu twite acha hukumu waitoe wao

      Delete
    2. Mwenye blog na rage bado wanaumia na usajili wa mbuyu twite acha hukumu waitoe wao

      Delete
  8. Si walisema mkataba mpya walisajili fifa fifa inakuwaje fifa hawautambui shida ya kuongozwa na professor uchwara

    ReplyDelete
  9. Utopolo Hamna kitu, hamjui Sheria mashabiki na viongozi wenu.

    ReplyDelete
  10. Tatizo ni Msola. Anafanya kazi kwa nani? Tuanzie hapo!!!

    ReplyDelete
  11. Mmekuja wenyewe kusoma na kujazwa wenyewe na mmeamini alichokiandika....subilini

    ReplyDelete
    Replies
    1. endelea kuota ndoto za mchana...kwenye ile kamati ya TFF walikuwepo wanachama kutoka Simba na Yanga...na Mwenyekiti mwana Yanga alijaribu kupindisha haki kwa siku tatu ikashindikana...jee Yanga wametuma kipande cha karatasi chenye sahihi kilichochanwa?

      Delete
  12. Vijana ingieni kwenye mtandao wa FIFA. Viongozi wetu wanatuhadaa.

    ReplyDelete
  13. Rage matako ya mama yake kwani alipotuita mashabiki wa simba mbumbumbu alikuwa hajuhi sheria?Kwanza simpendi ndio maana tulilikata jina lake mapema kwenye kamati ya uchaguzi Tabora kwa kukumbuka ushenzi aliotufanyia wana simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic