August 25, 2020

 

KLABU ya Yanga, imeanza sherehe zao kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo uzinduzi ulifanyika rasmi jijini Dodoma Agosti 22 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa klabu hiyo na wanachama wao.

Kilele cha Wiki ya Wananchi kinatarajiwa kuwa Agosti 30, Uwanja wa Mkapa na inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya  Eaglenor ya Burundi.


Katika uzinduzi huo, yalifanyika maandamano ya amani kuanzia Uwanja wa Jamhuri na kumalizikia Viwanja vya Mashujaa jijini humo.Lengo la maandamano hayo ni kuwa karibu na wananchi pamoja na kusaidia jamii katika uchangiaji wa damu.


Zoezi la kuchangia damu lilifanyika katika Viwanja vya Mashujaa likiongozwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msola, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa, Suma Mwaitenda, Ofisa Mhamasishaji, Antonio Nugaz na wengineo.

 

Katika hatua nyingine, Yanga inatarajiwa kupambana na Coastal Union katika mchezo maalum wa Kombe la GSM utakaochezwa Agosti 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

 

Katibu Mkuu wa Coastal Union, Rashid Mgweno, alisema: “Mchezo huu wa GSM Cup umetokana na makubaliano ya mauzo ya mchezaji, Bakari Nondo Mwamnyeto ambao unaweza kuwa endelevu kwa miaka ijayo na itaweza kushirikisha timu mbalimbali.”

8 COMMENTS:

  1. Enter your comment...tuko tayari wana yanga.

    ReplyDelete
  2. GSM kweli nyoko kesha waona Yanga madunya kaamua kuanza kucheza na akili zao kaanzisha kombe la GSM alafu kaamua kucheza na COAST akijuwa lazima atawafunga na kulichukua na kuanza kutamba kwenye media na title za kufarijiana YANGA YAANZA KUBEBA MAKOMBA , YANGA YAFUNGUA AKAUNTI YA MAKOMBE akijuwa atawafanya wanaYANGA wanafurahi na kuhisi wanakwenda kutamba kwenye ligi...Kwa kikosi cha YANGA ni bora kwa kwenda kugombania nafasi ya 2 na 3 lakini siyo UBINGWA.

    ReplyDelete
  3. Tulilataa matusi ,kama Elimu yako ya ustarabu ni ndogo nenda kapige chabo,huna lugha nzuri na kwanini uishi kwa kudhania una uhakika kwani GSM ni KIONGOZI YANGA?halafu wengi huku kwenye michezo ndo mnaona pa kutukania why?

    ReplyDelete
  4. Wewe unayejua hayo yote si ukadhamini tuone.Mimi wewe upo kwenye makundi mawili 1.Ni Simba unaona wivu au 2.Ni Yanga maslahi umebanwa na safari tunaondoa mpaka Makomando tuone

    ReplyDelete
  5. Huo uchungu wa mpira ungekuwa Ni kwa Nchi Wengine humu wangepewa nchi baada ya Magufuli kumaliza muda wake maana mpaka inashangaza

    ReplyDelete
  6. Kwani hao walowaletea Vitalo kwa mkwara wakashinda sita wakashangilia si wamepita? wanaendelea kutamba kwa uongo utadhani watu hatuna taarifa za Football Duniani,mlokwenda mmepigwa wajanja walibaki kuangalizie Tv .Sasa wewe Kama umeshtuka kwanini upandishe nyongo ya mwili kwa matusi badala ya kukaa kimya au kusema Amina?uliona viwanja viwili kujaa hii si afadhali ya last year?

    ReplyDelete
  7. Damu wachangie watu wa Dododma halafu mechi ya kilele waangalie watu wa Dar! Dunia haina usawa

    ReplyDelete
  8. Sio Kila kitu kuiga team ya Burundi tena?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic