August 28, 2020

 


RASHID Juma, winga wa Simba amejiunga na Klabu ya Polisi Tanzania kwa mkopo kwa wa mwaka mmoja.


Nyota huyo msimu wa 2020/21 atakuwa ndani ya Polisi Tanzania yenye maskani yake Kilimanjaro.


Ndani ya Simba ambao ni mabingwa watetezi hakupata nafasi ya kuwika kwa msimu wa 2019/20 kutokana na ufinyu wa namba.


Pia ilipaswa atolewe kwa mkopo msimu uliopita ila nyota huyo inaelezwa kuwa hakuwa tayari ila msimu huu amekubali kuibukia ndani ya Polisi Tanzania .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic