KELVIN Yondani beki mkongwe ndani ya Klabu ya Yanga ambaye aliachwa jumla baada ya mkataba wake kuisha inaeelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na mabosi wake hao ili arejee kikosini.
Yondani aliachwa pamoja na beki wa kulia Juma Abdul ambao kwa nyakati tofauti ndani ya Yanga waliwahi kuvaa kitambaa cha unahodha.
Sababu ya kuachwa ni kushindwa kuelewana kwenye masuala ya kimkataba jambo lililofanya pande zote mbili kukubaliana kila mmoja aendelee na maisha yake.
Abdul mpaka anaachwa na Yanga baada ya mkataba wake kuisha alikuwa ni nahodha msaidizi.
Habari zinaeleza kuwa kwa sasa mabosi wa Yanga wameanza kufanya mazungumzo na Yondani ili kumrejesha ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuendelea kupambana kwa msimu wa 2020/21.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli hivi karibuni alisema kuwa timu ipo imara kwenye usajili na ikiwa itahitaji saini ya nyota yoyote yule ni rahisi kumpata kwa kuwa wanajiamini.
"Mchezaji ambaye tutakuwa na malengo naye ni rahisi kwetu kumpata kwa kuwa uwezo tunao na tunatambua kwamba malengo yetu yapo kwenye jambo gani, bado tunaendelea na usajili hivyo wachezaji wetu wote tutawatambulisha Agosti 30 Uwanja wa Mkapa,".
Wamekosa wachezaji wa nje waliowategemea wamerudi kwa akina yondani. Usitukane mamba ili hali hujavuka mto
ReplyDeleteUnasemaje uwezo mnao wakati akina yondani walihitaji 30ml tu.
ReplyDeleteWeye Jana ulicheza na kitimu ambacho kinahistoria kufungwa mechi kibao ukatudanganya eti mechi ya kimataifa��������������
ReplyDeleteYondani wa nini tena wakati tuna Mwamnyeto tuliyempa milioni 200 za usajili?
ReplyDeleteNamshauri Cotton juice atafute changamoto mpya kwenye timu itakaypheshimu kipaji chake. Yanga ilshamwacha asirudi nyuma watamdharau zaidi
Deleteukiona hvyo ina mwanyento haminiki hahahahahahha
ReplyDeleteDah!utopolo mnaiga wakati hamwezi, ninyi level yenu ni Amina yondani na mkivuka sana zenji na Kenya *utopolo Ni utopolo tu pesa Hamna mjikubali msiige mtaumia.* Wanaume tunacheeeja 😆😆😆
ReplyDeleteUnawashwa washwa?
DeleteWewe mkiya fc anga zako za mazembe al ahly zamalek lkn usajili wako wote ulofanya wachezaji walomaliza mkataba latika team zao huna uwezo wa kununua wa kuvunja mkataba na hizo team
DeleteHao wachezaji wasio na uchungu na timu wanarudishwa kwa nini?!!
ReplyDeleteYondani; Juma Abdul na Ngasa walipaswa kuachwa kwa heshima siyo hivyo walivyofanyiwa.
ReplyDeleteWanakula matapishi yao tena hawana lolote hao kandambili aka vyura aka GONGOWAZI
ReplyDeleteDuh mapovu ya nini?
DeleteKwanza wewe huna hela, mdomo tuu
Delete