August 23, 2020

 

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Harrison Mwakyembe, ni mgeni rasmi wa Tamasha la Azam FC Festival, leo Agosti 23.


Mwakyembe yupo kwa niaba yaWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye amepata udhuru alitarajiwa awali kuwa mgeni rasmi.


Mwakyembe yupo jukwaa kuu akiwa na Mkurugenzi wa Makampuni ya Bakhresa Group, Abubakar Bakhresa wakishuhudia burudani ambazo zinaendelea ndani ya Uwanja wa Azam Complex.


Tayari wachezaji wapya na wale ambao walikuwa na kikosi msimu wa 2019/20 wameshatambulishwa.

David Kissu kipa kutoka Gor Mahia ndiye anakuwa kipa namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC huku namba mbili akiwa ni Benedickt Haule.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba atafanya makamuzi baadaye kidogo baada ya mechi ya kirafiki kati ya Azam FC na Namungo FC inayotarajiwa kuanza muda mfupi ujao.

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic