August 28, 2020


INJINIA Hersi Said, Mkurugenzi wa Masuala ya Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa kwa sasa timu hiyo imefunga hesabu za wachezaji wa ndani na mpango uliopo ni kuboresha kikosi kwa kuleta wachezaji wa kimataifa.

Ilikuwa ikielezwa kuwa Yanga ipo kwenye mazungumzo na nyota wao wa zamani, Juma Abdul na Kelvin Yondani ambao mikataba yao ilikwishwa na walishindwana kwenye masuala ya kuongeza mikataba upya.

Hersi ameweka wazi suala hilo kwa kusema kuwa:"Hakuna hesabu za kuwaleta wachezaji wa ndani kwa sasa kwa kuwa tayari tumeshafunga hesabu zao hivyo hatuna mpango wa kuwasajili wachezaji ambao tulishaachana nao.

"Ni wachezaji wazuri na tunawaheshimu lakini hakuna nafasi ndani ya Yanga, kwa sasa tunafikiria kuleta wachezaji wakigeni ili kufunga mjadala wa kuleta wachezaji na kufanya maandalizi mengine ndani ya timu," amesema.

Chanzo:Wasafi

4 COMMENTS:

  1. Kuna mtu ulipotoa habari ya Yondani kurudi alimwaga upupu,eti usitukane mamba hapa Mimi shida na akili zetu ,kweli ukiangalia mawazo yanayotoka humu inakupa picha ni aina gani ya Watu sisi ,kifupi fikra zetu Ni finyu .Wakati mwingine mwandishi anatoa habari akitegemea apate maoni zaidi yaliyo chanya lkn sisi Waswahili hata habari haikuhusu ilimradi unamtazamo hasi Ni kubeza tu Why ???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nawewe umeingia kwenye mkumbo huo huo wa kulalamika badala ya positive thinking!

      Delete
  2. Ni kweli nimeingia lkn mengine tunakaa kimya,ila ukweli ambalo sitaacha kulalamika ni ninyi watu wa media kutokuwa Wazalendi,mkuuu kweli nikae kimya pale unapomlinganisha Molinga na nchimbi eti kisa Magoli ,?Nchimbi mchezaji wa National Team ya Tz unakubali kumfananisha na huyo jamaa nisilalamike.kwangu ndilo jukwaa la kuwapata .Ukweli Team yoyote inayocheza na Yanga ikiwa na Molinga Ni sawa unacheza na Timu pungufu,mechi zote tulipata matokeo against Simba hakuwahi kuvaa hata jezi,Ni mzigo Uwanjani workrate yake ni below standard naturally

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mechi ngapi ulishinda against Simba? Ni moja tu. Au na draw umehesabu? Kumbuka mechi mliyofungwa 4 ni matokeo ya Molinga kuangushwa pembeni kidogo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic