August 10, 2020



BAADA ya picha ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa kuonekana akiwa na watu wa Yanga ikiwa ni pamoja na Injinia, Hersi Said inaelezwa kuwa tayari wameshaanza kufanya masuala yake taratibu kuingia mtaa wa pili.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa wameanza kazi taratibu kujibu mapigo ndani ya mtaa wa pili hivyo mengine yanakuja:- "Ni kweli kuna picha ambayo imeonekana na alikuwa ni Senzo lakini siwezi kuzungumzia alikuwa anafanya nini.

"Ukitaka kuchukua vifaranga anza na mama kwanza kisha wengine watafuata ndivyo ilivyo hivyo tumeanza na mama kisha vifaranga vitafuata.

"Tumekuwa na utaratibu wa kuchukua wachezaji wetu kutoka kwetu na wao pia wamekuwa wakichukua wachezaji kwetu, walimchukua Niyonzima, Gadiel ila hatujasema kitu nasi pia tulikuwa tunachukua wachezaji wao.

"Lakini kuna watu ambao wamekuwa na ukorofi na wanavuruga mpira, sisi tuliokuwa tumekaa mafichoni sasa tumeamka ili tuonyeshane nani atalia ama atacheka," ilieleza taarifa hiyo.


9 COMMENTS:

  1. Ni kama jamaa aliyejisifu kwa kutembea na house girl wa jirani yake na jirani akajibu mapigo kwa kutembea na mke wa jamaa..........

    ReplyDelete
  2. Senzo si ndo anayeenda kucheza namba tisa pale badala ya Molinga yanga itakuwa moto kweli

    ReplyDelete
  3. Wanaosema eti Simba imefanya vizuri zaidi kipindi cha Senzo wanajidanganya..Ki uhalisia mwaka uliopita Simba ilikuwa na mafanikio zaidi kisoka na huyo kocha Sven aliyemleta amaesaidiwa sana na Matola..Wote tunajua timu ilivyokuwa inaboronga wakati alipoamua kuendesha timu bila ya collaboration na Matola.Wao kama Yanga wameona Senzo ndiyo mali basi wamchukue..vitu viwili ni dhahiri hawataweza mlipa mshahara aliokuwa anapata Simba bila kuwaumiza wachezaji mfano kuwacheleweshea mishahara au kuendesha dhuruma..Pili haendi pale kuchukua nafasi ya Morrison..Kwako Senzo nenda salama!Asante kwa huduma yako

    ReplyDelete
  4. Simba ilifanya vizuri zaidi kipindi cha Aussen na Magori kuliko cha Senzo na Sven..tuache porojo

    ReplyDelete
  5. Siku zote mwanaume akishaanza kutoka nje ya ndoa mwanamke akijua basi atataka kulipiza ili amuumize mume wake, kwa hiyo sisi simba tumeona tuwape tu wake zetu mali zetu kidogo ili huko wanapoenda kuanzisha maisha mengine wasipate tabu saaaaaaaaaana aah aah aah aah simba bwana noma kweli

    ReplyDelete
  6. Kumchukua Senzo ....akili za Yanga hizo..Na labda leo pale maamuzi ya TFF yakitoka tutajifunza zaidi pale akili za Yanga zinapoishia!Sydney, Balinya, Yikpe, Molinga, Haruna, Sibomana hawakupata miaka miwili...Ni nini kilifanya Yanga wampe Morrison mkataba miaka miwili? Je ni kwamba yeye alikuwa anapata mshahara mdogo sana hivyo Yanga wakaona wanamudu malipo hivyo kumlipa miaka miwili si shida? Hadi muda wanapodai walimuongezea mkataba panapo mwezi wa tano alikuwa kafunga goli 2 assist 2 tu.Sasa hiyo siyo sababu ya kumpa mchezaji wa nje aliyecheza karibu miezi sita mkataba wa miaka miwili!.Au ni vile alikuwa anatembea juu ya mpira ndiyo Yanga walimuongezea miwili?akili zao hizo..kuna uwezekano aliyosema Eymael yana ukweli kidogo.Kwa hakili ndogo na rahisi haiingii akilini Yanga walifikiaje maamuzi ya kumpa mkataba wa miaka miwili kwani wengine wakigeni waliokuwa wanafanya vizuri zaidi hawakupata!.kwani morrison alikuwa hajaonyesha skills za miaka miwili. Au ni lile gori ambalo saleh jembe waliamua kumpa jina na kuendelea kuimba kila siku na kuandika kila siku Muuaji wa Simba ...hadi 4G ilipotua.Hatujasikua tena huo wimbo

    Ukitaka kujua ustaarabu wa Jangwani angalia picha inayoendelea kwz Tshishimbi,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umekurupuka kuandka 🙄
      Na inaonesha umeandika ukiwa na mihemko mikali Sana.

      Kwani Simba wao wamemsajili Morrison kwa takwim gn nzur unazozifikiria we??

      Pia kwa kipind hicho FUNDI MITSON ALIKUA ANA TAKWIM GAN MBELE YA Morrison?? Je hakustahil kua bora

      Delete
  7. Simba povuuuuu. Tunawadere tu. Sizitaki mbivu hizi fyuuuuuuuuuuu... MSITUFOKEE

    ReplyDelete
  8. Simba hawatoi povu bali wanawashangaa nyinyi mnaoona kama klabu yenu sasa imekuwa ka Real Madrid baada ya kuja huyo senzo klabu ili iwe kubwa kama Tp Mazembe, Al Ahly sio kuwa na mtu kama senzo tu peke yake kuna vitu vingi sasa klabu hata uwanja wa mazoezi haina lkn hizo kelele mnazopiga,kama angekuwa yeye ni mtu muhimu sana kuna klabu kubwa kibao na zina watendaji kama yeye si wangemchukua tunaandika haya yote kwa kuwa mashabiki wa Manyani fc hamjielewi MA C.E.O wapo kibao duniani, Tp Mazembe inapata mafanikio C.E.O alikuwa ni Senzo? Al Ahly inapata mafanikio C.E.O ni senzo? sasa analetwa C.E.O mwingine Simba na maisha yanaendelea na simba inaenda kupata mafanikio kimataifa bila huyo senzo wendaazimu nyinyi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic