August 10, 2020


BAADA ya jana. Agosti 9 Senzo Mbatha aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba kutangaza kujiuzulu huku ikielezwa kuwa ameibukia kwa watani zao wa jadi Yanga, uongozi wa Simba umesema kuwa masiha lazima yaendelee.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara  amesema: "Ameondoka yeye lakini timu si inabaki kuendelea na maisha yake kwani ameondoka na timu? Simba ni kubwa kuliko mtu yoyote ameondoka hatumsemi vibaya shughuli zitaendelea hakuna jambo lolote ambalo linatutikisa.

"Simba ipo muda mrefu kabla ya Senzo, hata kama ameondoka bado Simba itazidi kuendelea kuwepo hakuna shabiki ambaye alitikisika hakuna kiongozi ambaye alitikisika," amesema. 


Chanzo:Wasafi FM

7 COMMENTS:

  1. Haujapngea Uongozi pale no Haji Manara Fc maana mnamwamini Sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Manara ndiyo afisa habari wa Simba, taarifa zote za simba zinatakiwa kutolewa na Manara. Kama kila kiongozi anatakiwa kutoa habari basi hakuna haja ya kuwa na afisa habari au msemaji.

      Delete
  2. Huyu Haji Manara ndo chanzo cha chokochoko zote maana anajifanya ni mjuvi wa mambo kuwazidi wenye majukumu yao,yaani utadhani yeye ndo CEO wa timu kumbe ni kidampa tu

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo mlikuwa mnataka aseme imetuuma sana Simba kwa Senzo kuondoka na kwenda Yanga nyie ni wendawazimu kweli kama ma C.E.O wameisha duniani basi tutaona, kinashuka kitu kingine zaidi ya huo uchafu wenu sijui senzo sijui nani alafu kama kawa simba Robo rfainali klabu bingwa Africa kama kifo na binadamu msimu huu manyani nyie

    ReplyDelete
  4. Inaonekana kuna watu hawajui C.E.O maana yake nini na majukumu yake ni nini? Huyu ni mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za klabu. Huyu ni sawa na mtendaji mkuu wa bodi au katibu mkuu wa Tff. yeye ni mtekelezaji tu wa sera na maamuzi ya klabu yanayoamuliwa na bodi ya wakurugenzi. endapo maamuzi ya bodi ni mabovu huyo hawezi kuisaidia chochote klabu. Pesa za usajili hatoi yeye wala mishahara hatoi yeye hana mamlaka yoyote ya kuamua ni lipi na lipi litekelezwe. Hayo ni maamuzi ya bodi. Kama klabu ina mafanikio basi ni kwa kuwa bodi ilifanya maamuzi sahihi. Mchango wa CEO ni kwenye utekelezaji tu wa maamuzi.

    ReplyDelete
  5. Senzo atakuwa mshambuliaji utopolo"Yanga""yeboyebo""gongo wazi""vibonde wa mnyama Simba" FC na kuendelea kuwa wamchangani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic