AFC Arusha, leo Septemba 8 imemtangaza Atuga Manyundo kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo inayojiandaa na michuano ya Ligi Daraja la Kwanza ,Tanzania bara.
Manyundo atasaidiwa na kocha, Abdallah Juma kukinoa kikosi hicho chenye maskani yake jijini Arusha.
Manyundo aliwahi kukinoa kikosi cha Mashujaa FC ya Kigoma ambapo iliwatungua Simba mabao 3-2 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Mkapa.
Pia aliwahi kuifundisha Stand United iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ila msimu huu itashiriki Ligi Daraja la Pili kwa kuwa ilishuka pia kwa kuwa ilimaliza kundi B ikiwa nafasi ya 10 na pointi 24.
Buriani stendi United tutaonana Wana shinyanga wakipenda
ReplyDelete