September 18, 2020

 


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, ameonekana kuwa na maisha magumu ndani ya kikosi cha Simba, hii ni baada ya kutokuwa na uhakika wa kumaliza dakika tisini kama ilivyokuwa anaitumikia Yanga.

 

Morrison ambaye amejiunga na Simba msimu huu baada ya kumaliza mkataba wa miezi sita ndani ya Yanga, mpaka sasa amefanikiwa kucheza mechi tatu za kimashindano ndani ya kikosi hicho.

 

Katika mechi hizo, amefunga mabao mawili, bao moja nafasi moja ya bao.Katika mechi hizo zote, Morrison hakutoboa dakika tisini na kushuhudia akiishia dakika 60 tu.


Katika mechi ya kwanza ya Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Morrison alitoka dakika ya 66 na kuingia Rally Bwalya. Simba ilishinda 2-0.

 

Mechi ya pili ilikuwa ni kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu iliyochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kumalizika kwa Simba kushinda 2-1. Morrison alitoka dakika ya 67, nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Ajibu.

 

Kiungo huyo aliyekuwa maarufu ndani ya Yanga kiasi cha kucheza muda mwingi kwenye mechi zake ndani ya Yanga, wakati Simba ikitoka sare ya 1-1 na Mtibwa kwenye Ligi Kuu Bara mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, alitoka dakika ya 66, akaingia Meddie Kagere.

 

Kocha Sven amezungumzia hilo akisema: “Katika kikosi changu, kila mchezaji ana nafasi ya kucheza, nina kikosi kipana, hivyo nawapa nafasi wote kuona uwezo wao kabla ya kupata kikosi cha kwanza cha uhakika.”

20 COMMENTS:

  1. reasoning skill yako ni ndogo sana..hujui kusasambua na kusanikisha..Morrison hamilizi dak 90 sababu kuna wachezaji wengine wazuri benchu wanapaswa kuingia..Yanga hawana kikosi kipana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kutomaliza dk 90 si jambo laajabu hata Yanga mechi zingine Morrison alikuwa hamalizi na akitolewa anawaka ama anatoka nje ya uwanja moja kwa moja!!!

      Delete
    2. Acha mawazo mgando kaka,nini maana ya kikosi kipana? kwa sasa huyo benard anakoelekea ni kusugua bench tu,na hapo ndipomtakapojuta kumchukuwa kwa garama kubwa halaf hatoi mchango unaoendana na usajil wake

      Delete
  2. Yanga Ni Yanga na Simba Ni simba. Utopolo hawana wachezaji wenye viwango Kama Simba ndo yanamkuta haya. Simba wote Ni wakali ukipata hata dk 3 kucheza mshukuru MUNGU.

    ReplyDelete
  3. Mbona Barcelona wote ni wakali,lakini ulishawahi kumwona MESSI akitolewa. Morrison yatamkuta ya Ajibu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huangaliagi mpira kaa kimya. Mess hatolewagi?

      Delete
  4. Simba haina mchezaji mzuri hata mmoja wa kihivyo mipango mingi Sana hapa subiri tukinganganiana Sana juu wataanza mikutano bar Kama ile ya Sumbawanga ilo wasaidia kumpata Morrison .Kale Kanunda kameoa juzi mechi na Mtibwa utadhani kalitoka kujichua/master

    ReplyDelete
  5. Morrison akiwekwa benchi ambaye ndo Usajili bora kwenu hao wengine si bora warudishe pesa?ndo maana Hans pope anaanza kujitetea amewaingiza mkenge Mgalu babu ,Bwalya hovyo,Onyango huliona uzee hata kuruka taabu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba makombe tu, utopolo maneno tu. Mwenye akili achague atake makombe aje msimbazi atake maneno ya taarab aende utopolo.

      Delete
  6. Ila Yanga punguzeni mdomo. Simba sare mmoja na kashinda mmoja. Yanga sare mmoja kashinda mmjoa sasa inaonekana kama Yanga ndo anaongoza ligi na mechi zimebaki chache. Ligi ndo kwanza inaanza maneno ya nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. True! waambie utopolo hao wanaona kana kwamba washachukua kombe 2020/21

      Delete
  7. Morison staili yake ya uchezaji ni winga asa kwa mfumo wanaocheza simba wa kutumia viungo wenge kwenye baadhi ya viwanja ambavyo eneo la kuchezea ni dogo na havina ubora hasa vya mikoani atapata taabu sanaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona hata hapa dar perfomance yake yakusuasua tu,huyo jamaa ni kimeo ndio maana ananyodo sana,mchezaji mzuri hutakiwi kuwa na nyodo,muone chama bonge la mchezaji lkn hana makuu,lkn huyo kipusa bongo ataiona chungu kabla ya second round..

      Delete
  8. kwani hii habari yanga ndo wameposti??

    ReplyDelete
  9. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  10. Waandishi wengine viazi kweli chaajabu nn hapo?mfungaji bora WA misimu miwili mfululizo anaanzia bench utakuwa Morrison?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic