September 12, 2020

 


JANA Septemba 11, Yanga ilizindua rasmi jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2020/21 ambazo zitaanza kutumika rasmi kwa wachezaji wake kesho, Septemba 13 mbele ya Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

Jezi hizo zilipozinduliwa mashabiki wengi walijitokeza kuzinunua makao makuu ya Jangwani ambapo pia duka la jezi lilizinduliwa siku hiyo

Pichani ni viongozi ndani ya Yanga ambapo ni Injinia Hersi Said, Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya Klabu ya Yanga yeye ametupia jezi ya njano na mshauri mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha yeye ametupia jezi rangi ya kijani.

Akizungumzia kuhusu jezi mpya, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amewataka mashabiki kuendelea kununua jezi ili kuipa sapoti timu yao na kuendeleza uzalendo.

"Mashabiki waendelee kununua jezi kwani zipo tayari zimeshafika na tutapeleka kwenye maduka mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kariakoo, Mwenge ili kuweza kuwafikia mashabiki na wadau.

"Pia kwa wale wa mikoani wasiwe na mashaka jezi zitapelekwa kwani kwa sasa mambo yanawekwa sawa hivyo wasiwe na mashaka," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic