September 4, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu utakaopigwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine.


Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Simba na Ihefu ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ambayo itaanza kutimua vumbi rasmi Septemba 6.


Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanahitaji ushindi ili kupata pointi tatu muhimu.


"Maandalizi ya kikosi yapo sawa na kwetu sisi baada ya kumaliza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC ilikuwa ni ishara kwamba tayari tumeshaanza Vita kutafuta ushindi kwenye mechi zetu,".


Mchezo wa Ngao ya Jamii ulichezwa Agosti 30 kati ya Simba na Namungo FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.


Simba ni mabingwa watetezi wameshaanza mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ikikutana na  Ihefu ambayo imetoka kupanda daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

8 COMMENTS:

  1. vita ni vita ...wasiichukulie powa Ihefu

    ReplyDelete
  2. Kila la kheri na tuendelee na ubingwa wetu kwani tupo sawa kuliko miaka yote iliyopita. Nidhamu iendelee ndio iliyotufikisha hapa tulipo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa najua ako katimu kadogo hamtawagribu hao wachezaji na hamjamtafuta refa wa mechi.

      Delete
    2. Mmeshaanza malalamiko

      Delete
  3. Hii inadhihirisha kuwa Simba ni bingwa tayari msimu huu ukishaanza kuona hadi washabiki wao wanaanza maneno ya simba kununua mechi, mara kuwaghiribu marefa manake wameshashindwa kucheza mpira uwanjani sasa wanataka kucheza mpira mitandaoni wamesahau mechi yao na polisi kilichotokea mechi yao Kagera sugar kilichotokea, mechi yao na Lipuli kilichotokea. Tuendelee kuwakeraaaa tu mapaka wakome!

    ReplyDelete
  4. Utopolo mbona visingizio mapema sana hata mambo hayajaanza?

    ReplyDelete
  5. Kocha apange kulingana na mahitaji ya mechi hasiangalie jina








    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic