KESHO
Jumapili, Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 unatarajiwa kuanza ambapo
zitachezwa mechi saba, kisha Jumatatu zitamalizia tatu kukamilisha raundi ya
kwanza.
Jumla ya
timu 18 zitashiriki ligi hiyo kwa msimu huu ambapo zimepunguzwa kutoka 20
zilizokuwa kwa misimu miwili iliyopita.
Punguzo la
timu limekuja likiwa na lengo la kuona ushindani unakuwa mkubwa zaidi, hii ni
baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuona kuwa na lundo la timu halafu
zingine zinalia njaa, si sawa.
Kikubwa kila
mmoja wetu anahitaji kuona ushindani kuanzia ndani hadi nje ya uwanja. Hayo
yote yanawezekana kama timu zote zitajimudu.
Kuwa na
lundo la timu kwenye ligi kisha mambo yakaenda ndivyo sivyo, ndiyo mwisho wa
siku tunakuja kushuhudia timu zingine zikiwa hatarini kumaliza ligi kwa sababu
ya ukata.
Mifano ipo
mingi, hii ishu ya timu kushindwa kujimudu katika ligi na kuanza kulialia njaa
lipo kwa misimu mingi. Lakini kwa misimu miwili iliyopita lilikithiri sana,
hivyo basi imani yangu ni kwamba msimu huu hatutakuwa na vilio vingi.
Wadhamini
wakuu wa ligi hiyo, Kampuni ya Vodacom, kwa miaka mingi wamekuwa wakiidhamini
ligi hiyo kiasi cha kuondoa yale makali ya klabu kujiendesha, lakini
ilipojiweka kando, hali ilikuwa mbaya sana.
Kuanza kwa
ligi hapo kesho, kuwe na mambo mengi mapya, wadau wa soka tunahitaji kuona
mabadiliko makubwa sana kuanzia kwa wachezaji, mabenchi ya ufundi hadi
mashabiki.
Kwa
wachezaji, mnapaswa kucheza kwa viwango vya juu, kuwa kwenye kikosi cha timu
uliopo kwa sasa si kwa bahati mbaya, makocha wameona uwezo kwamba unaweza
kuisaidia timu, hivyo lipa imani hiyo kutoka kwa makocha wako.
Itakuwa ni
aibu kwako kucheza kama umelazimishwa wakati hiyo ni kazi yako. Kila mmoja
aifanye kazi yake ipasavyo, hapo mtaona matunda mazuri ndani ya timu yenu.
Kwa benchi
la ufundi, suala la kupanga kikosi liwe la kufuata weledi, kusiwe na vinyongo
kwa sababu tumekuwa tukisikia sana kwamba wachezaji wakiwa na sintofahamu na
makocha wao, basi benchi linakuwa makazi yao.
Kikubwa
suala la ugomvi wenu wa nje ya uwanja msiulete kwenye timu, itawagharimu sana
tu, linapofika suala la kazi, wekeni tofauti zenu pembeni, mtafanikiwa.
Mashabiki na
nyinyi muwe na umoja na mshikamano katika kuzisapoti timu zenu. Hakikisheni
mnakuwa kwa wingi viwanjani kuwapa sapoti wachezaji wenu wawape matokeo mazuri.
Wachezaji
wanapenda kuona mashabiki wao wanavyowasapoti, hapo huwa na nguvu zaidi ya
kupambana kuwapa matokeo mazuri ili mfurahi.
Kuna kauli
ya kwamba shabiki ni mchezaji wa 12, hivyo ikitokea mechi inachezwa halafu
mashabiki hawatoi sapoti, wachezaji wanashuka morali, mwisho wa siku wanapoteza
mechi.
Lakini
ikitokea siku timu imepoteza mechi, msianze kunyoosheana vidole, kaeni chini na
muangalie wapinzani wenu wapi waliwazidi nguvu, kisha jipangeni kwa wakati
ujao.
Kupoteza
mechi moja si mwisho wa safari, mnaweza kujipanga na kufanya vizuri mechi
zinazofuata, mwisho wa siku mnafikia malengo.
Yote kwa
yote niwatakie kila la heri katika mechi zenu na msimu kwa jumla. Tunataka
kuona mabadiliko ili soka letu likue zaidi.
Timu ziache visingizio. Ukifungwa kubsli matokeo. Baadhi ya timu ziache kudanganya wapenzi na wanachama wao.Tuanze utamaduni wa kusema ukweli.Tambo za magazetini hazileti ushindi.
ReplyDeleteKwa mawazo yangu; hiyo ligi bora ingechezwa Leo na kesho kuliko jumatatu.
ReplyDeleteJumatatu ni siku ya kazi tena ya mwanzo wa wiki, bodi ya ligi huwa siwaelewi kabisa
Bodi ya ligi sijui ilikuwa inafikiria nini
DeleteNa Kuna Jambo kingine la Venue ya fainali ya kombe la TFF. Unapopanga uwanja wa mikoa ya Katavi au Njombe,au Mara na mashindano yanahusisha timu za madaraja ya chini, what if zikaja kuingia fainali Kati ya timu hizo na mchezo ulishapanga kufanyika labda Kigoma?
DeleteKwa mtazamo wangu Venue yafya ingekua uwanja wa Mkapa then hizi timu ndogo zinakua zinapambana kucheza hapo Kama kivutio na motivation kwao.
Vilabu vyote ni sehemu ya bodi ya ligi hivyo vilishirikishwa kwa namna moja au nyingine kwenye maamuzi ya ratiba
Delete