September 7, 2020

 


KAGERA Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Mecky Mexime leo, Septemba 7, imeanza kwa kupokea kichapo mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.


Mchezo huo umechezwa,  Uwanja wa Kaitaba na kuwafanya mashabiki wa Kagera Sugar kushuhudia timu hiyo ikifungwa bao 1-0.


Bao pekee la ushindi kwa JKT Tanzania lilipachikwa kimiani na mshambuliaji wa timu hiyo, Adam Adam.


Bao hilo lililopachikwa dakika ya 16 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na kuwafanya Kagera Sugar kuyeyusha pointi tatu za mwanzo mazima.


Baada ya mchezo wa leo wanaanza kujiaandaa na mchezo dhidi ya Gwambina FC utakaopigwa Septemba 11. Inakutana na Gwambina FC ambayo nayo imetoka kunyooshwa kwa bao 1-0 mbele ya Biashara United ya Mara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic