September 11, 2020

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umeweza kuweka rekodi ya kuzindua jezi mpya pamoja na duka la vifaa ndani ya makao makuu ya timu hiyo yaliyopo mtaa wa Jangwani, Kariakoo.


Leo Septemba 11, Yanga imezindua jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2020/21 na mashabiki wengi pamoja na wadau walijitokeza kushuhudia uzinduzi huo na kuanza kununua jezi hizo.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kwa wale ambao watachakachua jezi hizo watakuwa matatani kwa kuwa wanashirikiana na mamlaka ya dola pamoja na mtandao mkubwa wa kufanya uchunguzi tofauti na msimu uliopita.


Mwakalebela amesema:"Tumekuwa timu ya kwanza kuzindua duka la vifaa vya Yanga pamoja na jezi nzuri na yenye ubora hivyo tupo imara katika kila idara na tunaamini kwamba tutafanya mengi makubwa.


"Mashabiki wametushangaza kwa kununua na kuzivaa jezi wakati huu tofauti na msimu uliopita na hii inamaanisha kwamba mashabiki wanaipenda timu na wanawekeza ndani ya timu na tunampango wa kusambaza jezi kwenye maduka mengine."

17 COMMENTS:

  1. Zinafaa kama zana ya kufundishia Jiografia shuleni

    ReplyDelete
  2. Duka ni la timu ya Yanga au ni la GSM ambao ndio wenye mkataba na makubaliano ya kuipatia Yanga jezi na vifaa vingine?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duka ni la Yanga sema jingine. Linamilikiwa na Klabu na ni mali ya Klabu....wamejengewa kwa hisani ya GSM...Lets swali jingine

      Delete
  3. Nitanunua kufundisha madogo shuleni maarifa ya jamii.

    ReplyDelete
  4. Hamna kitu hapo, jezi ipo chini ya kiwango, Bora ya kwanza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jezi ni bora na za kisasa we endelea kuumia...utaendelea "kukerwa" sana mwaka huu

      Delete
  5. Vyovyote iwavyo hamuwezi kuzilinganisha na za kwenu kama vitambaa vya waganga wa kienyeji maana bila ya shuka nyeupe na nyekundu mganga hafanyi kazi

    ReplyDelete
  6. Duh, Kuna watu wameumbwa kubisha tu, bila ya kuonesha vigezo vya vitu vizuri.

    ReplyDelete
  7. Jezi za Simba Kilo moja Elfu tano nenda Kariakoo uone,mbona hayo Matambala alowatengenzea Kassim Dewji yalipo toka na Hiyo mirangi ya Kichawi tulikaa kimya ,zetu mnatoa midomo Kama makahaba wanatafuta Wanaumme,kila mtu mpenZi.

    ReplyDelete
  8. Hyo Ni jezi za utopolo au ndo za kampeni CCM. Nashindwa kutofautisha CCM na utopolo.

    ReplyDelete
  9. CCm ilikuta Yanga ila mi nadhani Simba kapakatwa wowo mna wivu wa Kiswahili , best Kama hataki kasage chupa unywe jezi viwango Hiyo au toa mimba Kama una uchungu pole mikiaaaaa na Mo mkopesha pikipiki .Nahitaji kilo nne za jezi za simba please

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtaishia kubadili jezi, sisi simba tunatwaa makombe tu. Mlipeni Zahera mshahara wake

      Delete
  10. Bora wewe wivu umekutoka cse povu la jezi limewazidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic