WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amesema hana tofauti wala chuki na Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, kama ambavyo wengi wanafikiria baada ya kuhoji juu ya uwekezaji wake wa Tsh bilioni 20.
Wikiendi iliyopita Kigwangalla alizua mijadala katika mitandao ya kijamii muda mchache baada ya kutangazwa kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez ,ambaye ametwaa nafasi iliyoachwa na Senzo Mazingiza aliyetimkia Klabu ya Yanga.
Akitolea ufafanuzi, Kigwangalla amesema; ”Sina matatizo na Dewji, yule ni rafiki yangu na pia alikuwa mbunge mwenzangu, nilishafanya naye biashara, suala la mkopo wa pikipiki wala siyo tatizo kwa kuwa nilimkopa, lakini alileta uswahili, mwanzo alikubali, baadaye alikataa.
“Lakini baadaye nilinunua kwa kuwa nilikuwa nataka kupeleka jimboni kwangu ili kukimbizana na muda, hivyo kama ningekuwa na chuki naye basi nisingerudi tena kununua bidhaa kwake.
“Suala la kuhoji Tsh bilioni 20 nilishawahi kufanya hivyo tangu mwezi Januari, hivyo baada ya kuona mambo kama hayaendi vile inavyotarajiwa, ilibidi niulize kwa kuwa niliona wanamuajiri Barbara ambaye ni mfanyakazi kutoka Taasisi ya Mohamed Dewji, maana yake hapo kutakuwa na tatizo kwa kuwa mchakato haujakamilika.”
Kigwangalla amesisitiza kwamba baada ya kuona baadhi ya wanachama na mashabiki wa Klabu ya Simba wamekasirika wakiamini anataka kumfukuza mwekezaji wao, sasa atakaa kimya ila ukweli utakuja kujulikana.
Ukweli gani utakaokuja kujulikana kwa kifupi jamaa chuki zake za kunyimwa huo mkopo ndizo zilizopelekea afanye hayo yote angekuwa anaipenda simba kweli asingeenda kwenye mitandao ya kijamii na kuhoji hizo bilioni ishirini bali angetumia sehemu sahihi kuhoji swala lake na majibu yasingejitosheleza angeenda kwenye mitandao ya kijamii hapo kidogo angeeleweka. Wabongo tuache chuki binafsi
ReplyDeleteTatizo njaaa ndio maana ukweli tunataka kuufanya uwongo hahaha
ReplyDeleteUmasikini kitu kibaya sana watu wakotayari hata kumkabidhi tajili wake zao akawatumia kisha awarudishie kisha wapewe pesa tu hahaha chapa ilale masikini hata awe na hoja za msingi ataonekana fara tu kwa sababu kamkosoa tajiri
ReplyDeleteWatu badala ya kuhoji mambo msingi wanahoji mambo binafsi issue ni 20 bilioni zimeshawekea
ReplyDeleteUmasikini mbaya sana. Simba nyie mnatishwa kidogo mnanyenyekea MO shame on u. Mnataka mheshimiwa akahojie wapi kama alitaka liwe private mbona mchakato haukuwa private. Wajinga ndio waliwao. Mkishtuka mhindi keshawatumia then anawabwagwa pwaaaaaaa na 20B hazipo.
ReplyDeleteGSM kdg tu aliwatishia, mlienda kumpigia magoti mpaka sasa anawapiga za uso mmenyamaza tu mnaugulia kimyakimya *kwa Morrison kawaliza,kwa bwalya kawaliza, kotei kawaliza,sure boy,shiboub,makambo kawaliza dah mengi ngoja niishia hapa kwa leo* kwa umaskini wenu utaendelea kuwaliza tu
DeleteLeo nimemsikiliza mshauri wa mo aliyekuwa CEO wa Simba kabla ya Senzo. Ameelezea vzr EFM radio ahsubuhi juu ya hizo billion 20 matumizi, mgawanyo na uteuzi wa CEO mpya. Hakika nimeelewa sana MO big up. Washamba na mafisadi watazudi kuongea na kubwabwaja wakichoka watanyamaza.
ReplyDeleteUtopolo mtofautishe MO siyo Manji.Manji katika mnayuyumba Kama make aliyetelekezwa na mumewe. Mo Wanasimba wenye akili tusonge mbele tuendelee kutwaa makombe.
ReplyDeleteGenge... oyoo..
ReplyDeleteWanasimba tusiwe na papara za yule mfuga kuku aliekuwa akitagiwa yai la dhahabu kila siku lakini tamaa ikamzidi mfugaji yule kutaka kuikomba zaidi dhahabu yote iliokuwemo kwenye tumbo la kuku ili atajirike haraka na ndipo alipoamua kuchukua maamuzi katili ya kumchinja kuku yule lakini matokeo yake alipoteza kuku yule na alikosa yai lile la dhahabu la kila siku na kuwa masikini zaidi kwani baada ya mfugaji kumchinja kuku yule alikosa yote. Hakuna asiejua kuwa Billion 20 ni nyingi kwa mimi na wewe tunaohitaji pikipiki lakini kwa Mo ni kama kukohoa vile.Na tumpongeze tu Mo kwani kabla ya mchakato wa kuingizwa B20 ishirini kwenye account ya simba tayari yeye aneahaanza kufanya yake tena makubwa tu kwa maendeleo ya simba ila sisi kama watanzania kila mtu anajifanya anajua kwani kuna hata baadhi ya watanzania wanaohoji kwanini Magufuli anaijenga nchi? Hakuna siejua kuwa Mo anakeereka kuona kuwa kwanini vilabu vyetu vimeshindwa kutwaa kombe la klabu bingwa Africa? Na ndipo alipoamua kuwa na malengo maalum ndani ya simba yaani special mission ya kuhakikisha kombe lile linatua kwenye ardhi ya tanzania na kwa kupitia klabu yake pendwa ya simba Mo ameamua kuekeza ndani ya simba ili kutimiza ndoto yake na ya watanzania waliowengi kuona tunatwaa kombe la klabu bingwa Africa kwa ngazi za vilabu na kama kuna Mtu au mtanzania anataka kupambana na Mo basi apambane nae katika hili yaani awe na wazo na uthubutu wa kuwa wa kwanza yeye na klabu yake kulileta taji la Klabu bingwa Africa tanzania kinyume ya hili tafadhali watanzania tuache majungu na Mo si wa kubezwa au kukatshwa tamaa ni wa kujengwa zaidi kiimani atuletee maendeleo ndani ya simba na Tanzania. Taifa linapambana kuwajengea mazingira bora wawekezaki hasa wazawa, hasa kwenye sekta ya michezo vipi lakini teba kula kukicha choko choko haziishi kwa Mo?
ReplyDeletePesa ndio mpango mzima, ukiwa huna pesa haiwezi kusikilizwa.
ReplyDeleteNdio maana matajiri wanafanya walitakalo kwasababu ya pesa.
Time will tell, which is which...
Tatizo watu wanasahau, Yanga walishapiga magoti kwa manji huku wanalia ili Manji aeendelee kuwa mwenyekiti Pale PTA Hall, na pia kuna mtu alimgusa GSM watu wakataka kuandamana ukweli ni kuwa mashabiki wa WIMBA na YANGA letu moja kama timu inafanya vizuri especially kwenye usajili, ukimgusa yule muwezeshaji basi ujue utaumia, mfano sasa hivi ajitokeze mtu aseme GSM aondoke uone mtiti wake watu wataandamana
ReplyDelete