VIVIER Bahati, Kocha msaidizi wa Klabu ya Azam FC ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara amesema kuwa wao hawahitaji mabao mengi ndani ya uwanja zaidi ya kupata pointi tatu muhimu
Hali ya timu ipo sawa na tatizo kwetu sio ushindi mkubwa ndani ya uwanja kikubwa ambacho tunakihitaji ni kupata pointi tatu muhimu.
"Ikitokea tukashinda kwa bao 1-0 uwanjani hio sio mbaya kwetu kikubwa ambacho tumekipanga ni kuona timu inapata pointi tatu muhimu mengine yatafuata.
"Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa leo dhidi ya Ihefu, tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tunahitaji pointi tatu ili kuendelea na rekodi ya kushinda mchezo wetu wa saba," amesema.
Azam FC imeshinda mechi zote sita za ligi ikiwa na pointi 18 kibindoni. Mchezo wake wa mwisho ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC inakutana na Ihefu FC ambayo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume.
Ihefu kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi sita ndani ya ligi ikipoteza mechi tano na imeshinda mechi moja ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Sokoine.
0 COMMENTS:
Post a Comment