October 17, 2020


 STRAIKA wa Azam FC, Prince Dube amefunguka kuwa hafurahii timu yake inapocheza kwenye baadhi ya viwanja vya mikoani kutokana na kwamba haviifanyi timu hiyo kucheza mpira ambao ameuzoea.

 

Straika huyo ameongeza kwamba katika viwanja hivyo pia wachezaji wanaovitumia wamekuwa wakitumia nguvu zaidi tofauti na wakikutana kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex.


Dube mwenye mabao sita katika Ligi Kuu Bara hadi sasa ameitumikia Azam FC michezo mwili mikoani dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine na dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

 

Straika huyo raia wa Zimbabwe amesema: “Mechi za Chamazi (Azam Complex) nazifurahia kwa sababu nimeshauzoea uwanja na ni rafiki kwa mchezaji yeyote.

 

“Lakini mkoani viwanja vyake ni vigumu kwa sababu haviko na usawa mzuri, vinasababisha timu kucheza mipira ya juu hivyo ni vigumu kufurahia mchezo mzuri wa pasi za chini, pia kuna matumizi makubwa sana ya nguvu,” amesema.


Azam FC ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi sita na imeshinda zote.


Safu ya ushambuliaji imefunga mabao 12 huku safu ya ulinzi ikiruhusu mabao mawili ndani ya msimu wa 2020/21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic