UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar utaamua hatma yao ya kuendelea na rekodi ambazo wameweka ndani ya ligi kwa msimu wa 20202/21.
Kikosi cha Azam FC kikiwa nafasi ya kwanza na pointi 21 baada ya kucheza mechi saba na kushinda zote, kesho, Oktoba 26 kinakutana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi saba.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:"Kikosi kimefika salama Morogoro na mchezo wetu wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar utatoa tathimini ya kile ambacho tumekifanya kwenye mechi zetu saba ambazo zimepita tukiwa tumeshinda.
"Sio mchezo mwepesi ninaamini kwamba utakuwa mgumu lakini wachezaji wanajua kwamba pointi tatu ni muhimu na wapo tayari kwa ajili ya hilo mashabiki watupe sapoti."
Kinara wao wa kufunga na kutengenza pasi ndani ya Azam FC ni Prince Dube ambaye amefunga mabao sita na kutoa jumla ya pasi nne za mabao.
Azam FC ikiwa imefunga jumla ya mabao 14 amehusika kwenye mabao 10.
0 COMMENTS:
Post a Comment