October 20, 2020

 


AYOUB Lyanga nyota wa Azam FC leo Oktoba 20 amefungua akaunti yake ya mabao ndani ya Ligi Kuu Bara wakati timu yake ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Ihefu, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


Bao la pili pia lilifungwa na nyota Idd Seleman, 'Naldo' dakika ya 83 ambaye naye amefungua akaunti ya mabao kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Azam FC ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, raia wa Romania.

Nyota wote wawili wamepachika mabao hayo kwa pasi za kinara wa kutupia ndani ya ligi, Prince Dube ambaye amefunga mabao sita na leo amefikisha jumla ya pasi nne za mabao ndani ya Azam FC.

Ushindi wa leo unakuwa ni wa saba mfululizo kwa Azam FC ndani ya Ligi Kuu Bara huku wakizidi kujenga ufalme wao nafasi ya kwanza kwa kufikisha jumla ya pointi 21.

Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu, mechi yake ya kwanza leo ameanza kwa kuonja joto ya jiwe kwa kuwa aliibukia ndani ya kikosi hicho Oktoba 18 akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar. 

Jana, Oktoba 19 timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar ilisepa na pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

3 COMMENTS:

  1. Azam FC wanaendelea kutoa statement....kwa mwaka huu wana jambo lao...mkifikiri huu ni moto wa mabua mwisho wa msimu Azam FC bingwa...mambo yamebadilika jamani

    ReplyDelete
  2. Tumekariri bila ya Simba na Yanga hakuna mpira.

    ReplyDelete
  3. Nyie acheni tuendelee kupigiana makelele tutakuja kushtukia azam fc ni bigwa wa ligi kuu ndo akili zitatusogea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic