October 20, 2020


 MSHAMBULIAJI namba moja ndani ya Simba, Meddie Kagere amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa anaweza kurejea uwanjani kwa kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania.

Kagere ndani ya Simba ambayo Oktoba 22 itacheza mechi ya ligi dhidi ya Tanzania Prisons ametupia mabao manne kati ya 14 ambayo yamefungwa na timu yake ataukosa mchezo huo sawa na John Bocco ambaye ni nahodha pamoja na Gerson Fraga ambao nao pia ni majeruhi ndani ya Simba.

Kagere amesema:”Kwa sasa ninaendelea vizuri na muda wowote kuanzia sasa nitarejea uwanjani kuendelea kupambana hivyo mashabiki wasiwe na mashaka katika hili,” .

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara Kagere atakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu ambapo anatarajiwa kurejea kwenye ubora wake Novemba 6.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic