October 22, 2020


 MABINGWA  watetezi wa Uefa Champions League, FC Bayern Munich wameendelea pale walipoishia msimu uliopita kuwa tishio katika michuano hiyo baada ya kupata ushindi mnono wa magoli  4-0 dhidi ya Atletico Madrid.

 

Bayern walikuwa wanacheza kwa kuwaonyesha vijana wa Diego Simeone kuwa ni mabingwa kweli wa michuano hiyo kwa jinsi walivyokuwa wanacheza kwa mamlaka wakiwa wametulia eneo la katikati licha ya kutokuwepo kiungo Thiago Alcantara aliyetimkia Liverpool.


Vijana hao wameonyesha kwamba pengo lake limezibwa vilivyo na Mjerumani Groetzeka.

 

Magoli ya FC Bayern Munich yamefungwa na Kingsley Coman dakika ya 28 na 72, Groetzka dakika ya 41 na Tolisso dakika ya 66 na kuifanya Bayern kuvuna pointi tatu zao za kwanza za Kundi A msimu wa 2020/21.

 

FC Bayern Munich chini ya kocha wao Hansi Flick, wanaendelea kuwa na wakati mzuri, huu ukiwa ni mchezo wao tisa mfululizo ya ligi ya mabigwa chini ya kocha huyo wakiwa wameshinda mechi zote na kufunga jumla ya magoli 34 na kufungwa magoli manne pekee.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic