October 22, 2020


 BEKI wa kulia wa zamani wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa safu ya ulinzi ya Yanga imetimia kwa ajili ya kupambana na washambuliaji wanaocheza katika ligi kuu kwa kuwa ni imara.

 

Juma Abdul baada ya kuondoka Yanga kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Inden FC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Zambia.

 

Beki huyo amesema kuwa amewatazama mabeki wote ambao wapo katika kikosi hicho na kugundua kuwa ni mabeki bora wa kuifanya timu hiyo iwe katika mikono salama dhidi ya washambuliaji hatari watakaokutana nao ndani ya ligi kuu.


“Yanga ina wachezaji wazuri haswa kwenye safu yake ya ulinzi, kuanzia mabeki wa kati hadi wale wa pembeni ni mabeki ambapo wametimia haswa tayari kwa ajili ya mapambano dhidi ya washambuliaji hatari wanaopatikana kwenye ligi kuu.

 

“Kuhusu Kibwana Shomari, ambaye anacheza katika nafasi ambayo nilikuwa nacheza mimi ya beki wa kulia, nampongeza kwa kuwa kuna kitu kakionyesha mpaka sasa, Kibwana ni kijana mdogo hivyo bado anayo nafasi kubwa ya kuzidi kujifunza, ila yupo vizuri,”alisema beki huyo.

1 COMMENTS:

  1. Inden fc inashliki ligi gan zambia au sielewi zambia zpo mbili mbna ligi kuu haipo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic