KOCHA Mkuu wa Biashara United ya Mara, Francis
Baraza amesema timu yake imejipanga kuhakikisha inapata matokeo katika mchezo
wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa leo Jumatatu mkoani Tanga.
Baraza amesema: “Kwa sasa naweza kusema najenga nyumba mpya baada kupata matokeo nyumbani.
"Tumejipanga kushinda dhidi
ya Coastal, tunaamini utakuwa mchezo mgumu kwani timu hiyo haijafanya vizuri
tangu kuanza kwa ligi ya msimu huu, tutajipanga kupata matokeo mazuri ambayo
yataiweka timu yetu kwenye nafasi za juu zaidi.
“Tutachukua tahadhari zote za kucheza ugenini lakini shabaha kubwa ni kupata mabao mengi katika mchezo huo.Kwa sasa kama timu tumeamua kila mchezo uwe fainali kwa kuhakikisha tunapata matokeo kwenye kila mchezo."
Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ili kurejea kwenye ubora kwa kuwa mwendo wao umekuwa ni wakusuasua.
0 COMMENTS:
Post a Comment