October 31, 2020


 MICHAEL Sarpong nyota wa kikosi cha Yanga leo ameibuka shujaa baada ya kufunga bao la ushindi mbele ya Biashara United na kuipa pointi tatu muhimu timu yake ambayo haijapoteza mchezo kwa msimu wa 2020/21.


Bao hilo la ushindi alipachika dakika ya 68 Uwanja wa Karume, Mara kwa kichwa akimalizia pasi ya nyota wa timu hiyo Ditram Nchimbi na kuituliza kasi ya wapinzani wao Biashara United jumlajumla.


Bao hilo linakuwa ni la pili kwa Sarpong ndani ya Ligi Kuu Bara huku likimfanya Nchimbi naye aandike rekodi yake ya kutoa pasi ya kwanza ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21.


Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 22 ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Azam FC ambayo ikiwa na pointi 22 ila zimetofautiana kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungana.


Azam FC imefunga mabao 15 na Yanga imefunga mabao 11 kwa upande wa mabao ya kufungwa Yanga imefungwa mabao mawili huku Azam FC ikiwa imefungwa mabao manne.


Biashara United inashuka nafasi ya nne ikiwa na pointi 16 ikishushwa kutoka nafasi ya tatu na Simba ambayo imeshinda leo na kufikisha pointi 16 tofauti ikiwa ni kwenye mabao ya kufunga ambapo Simba imefunga mabao 19 na Biashara United imefunga mabao 5.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic