October 31, 2020


LABDA unaweza kusema kwamba Simba bila Clatous Chama mambo yanaweza kuwa magumu ila mpira ndio matokeo yalivyo ndani ya uwanja.


Baada ya kucheza mechi mbili mfululizo bila kupata matokeo chanya kwa kuyeyusha pointi sita mazima ndani ya uwanja leo Oktoba 31 Simba imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui FC.


Mechi zake mbili ambazo ni dakika 180 ilichezeshwa ligwaride na Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela kwa kufungwa bao 1-0 kisha ikanyooshwa tena kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru na mechi zote mbili Chama hakuwepo kwa kuwa alikuwa anashughulikia paspoti na leo ameanza ndani ya kikosi cha kwanza na Simba ikasepa na pointi tatu.


 John Bocco nahodha wa Simba alipachika bao la kwanza dakika ya 25 na la pili alipachika dakika ya 64.


Ibrahim Ajibu kiungo mshambuliaji wa Simba amepachika bao lake la kwanza kwa msimu wa 2020/21 ndani ya ligi dakika ya 81 likiwa ni la tatu kwa timu yake leo sawa na Hassan Dilunga kiungo wa Simba ambaye amepachika bao lake la kwanza ndani ya kikosi hicho dakika ya 87 likiwa ni la nne.


Bao la kwanza la usiku kwa Simba ambalo lilikamilisha bao la 5 dhidi ya Mwadui lilipachikwa na nyota mwenye tabasamu lake kwa mbali, Said Ndemla dakika ya 90+3.

Mwadui inapoteza mchezo wake wa pili mfululizo na kufungwa jumla ya mabao 11 kwenye mechi mbili huku wao wakifunga bao moja.


Mechi iliyopita walifungwa mabao 6-1 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mwadui Complex na leo wamefungwa mabao 5-0 Uwanja wa Uhuru.


Simba inapanda kutoka nafasi ya nne mpaka ya tatu ikiwa na pointi 16 kibindoni na imefunga mabao 19 huku Mwadui FC ikiwa nafasi ya 15 na pointi tisa baada ya kucheza mechi 9 na ina pointi 9.

Ndemla naye amefungua akaunti ya mabao ndani ya Simba ambayo leo imeweza kusepa na pointi tatu mazima baada ya kuyeyusha pointi sita mechi zilizopita.

5 COMMENTS:

  1. JK Tanzania iliyo ifunga mwadui bao 6 tena ugenini,nayo ilikuwa na Chama? Mnaandika tu kuwadanganya wanasimba wajione timu imeimarika kumbe bado sana

    ReplyDelete
  2. Kuna watu wajiandae kisaikolojia 4G imerejea😀😀

    ReplyDelete
  3. Wameanza uwoga wanamuogopa chama

    ReplyDelete
  4. Ili biriani la Simba liive ni lazima mpishi Chama ahusike..full stop

    ReplyDelete
  5. Exactly simba ni chama mana mh ata mpira unaonekana akiwepo yeye but miqueson ni mchezaji mzuri sana japo yanga Atumtaki kabisaaa. Sis tunasepa na 1 goal with 3 points. Yanga i love u ever 💪💪

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic