October 8, 2020


 KELVIN John, nyota Mtanzania ambaye anakipiga nje ya nchi ndani ya Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambayo ilimpelekea kwenye kituo cha Brooke House ili akaongeze uwezo zaidi ametajwa kwenye orodha ya wachezaji 60 wenye vipaji duniani.

Kwenye orodha hiyo ambayo imeangazia wachezaji walioletwa duniani kuanzia mwaka 2003 na imechapishwa leo, Oktoba 18 imewaorodhesha wachezaji wengi wenye vipaji ikiwa ni pamoja na John.


Miongoni mwa wachezaji ambao wameorodheshwa ni pamoja na Luka Cveticanin wa FK Vozdovac, Israel Salazar anayekipiga Real Madrid,Nico Serrano anayekipiga Athelic Bilbao, Bruno Iglesias anayecheza Real Mdrid na Emil Roback anayekipiga Milan.


John amesema kuwa kwake ni furaha kuwa kwenye orodha hiyo ataongeza juhudi kufikia mafanikio zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic